
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Hospitali yaTaifa Muhimbili Bi. Priscilah Kinyamagoha akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Dkt. Harrieth Gabone Mwakilishi kutoka Shirika la Quality Health Care Solutions and Consulting (QHSCO) kutoka nchini Marekania akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mafunzo hayo.
Mmoja wa watoa mada kutoka Marekani akifundisha mafunzo hayo kwa vitendo.
Mafunzo hayo yakiendelea.
Na Angel Mndolwa
Shirika la Quality Health Care Solutions and Consulting (QHSCO) kutoka nchini Marekani linaendesha mafunzo ya siku nne kwa wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Amana, Hospitali ya Mwananyamala pamoja na na Kituo cha Afya cha Buguruni kuhusu namna ya kumsaidia kupumua mtoto ambaye amepata tatizo la kupumua baada ya kuzaliwa na mama aliyetokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo, Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga Muhimbili Bi. Priscilah Kinyamago amesema kuwa mafunzo yatakuwa ya vitendo zaidi kuliko nadharia lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu wanaohudumia mama na mtoto ili kupunguza vifo vya watoto wachanga na vifo vinavyotokana na uzazi.
“Asilimia kubwa ya vifo vya kina mama vinavyotokea baada ya uzazi vinatokana na kutokwa damu nyingi, wakati vifo vingi vya watoto wachanga vinasababishwa na tatizo la upumuaji, hivyo baada ya mafunzo tunaamini wataalamu wataenda kusaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto katika maeneo yao ya kazi” amesema Bi. Kinyamagoha
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Quality Health Care Solutions and Consulting (QHSCO) ambaye ni Mtanzania anayeishi Marekani Dkt. Harrieth Gabone amesema lengo la taasisi yake kuendesha mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi kwa wataalamu nchini ili kuboresha hali ya utoaji huduma.
Dkt. Gabone ambaye kwa taaluma ni muuguzi amesema amekuwa akiguswa na kutamani kusaidia nchi yake hasa katika eneo la uzazi.
Naye Dkt. Peter Yambe mshiriki kutoka Hospitali ya Mwananyamala amesema kuwa mafunzo yamewaongezea ujuzi kuhusu namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtoto anayezaliwa na changamoto ya upumuaji lakini pia mama aliyetokwa na damu nyingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...