Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WAZIRI wa afya Ummy Mwalimu ameeleza kati ya watu 100 Tanzania wanaoishi na virusi vya ukimwi 95 wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARVs) huku watano kati yao wanaacha dawa hizo ,suala ambalo linakwamisha juhudi za mapambano dhidi ya gonjwa hilo.

Aidha amewaasa , wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kutoacha kutumia dawa hizo na kuiasa jamii kuacha ngono zembe ili kujiepusha na maambukizi mapya ya Ukimwi.

Akizungumza na Wananchi katika kituo Cha Afya Disunyara na Mwendapole Kibaha mkoa wa Pwani, wakati alipoambatana na Mkurugenzi wa Mfuko wa kimataifa wa kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya (HIV), kifua kikuu (TB) na malaria (Global Fund) Peter Sand ,Ummy alieleza Kuwa ,hata Kama wanaona kuna unafuu wenye VVU wasiache matumizi ya dawa hizo .

Ummy alieleza, wanaona kuna kusuasua kwa matumizi ya dawa za ARV Kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi hivyo kusipokuwa na umakini wakati tunakaribia kuushinda tunaweza kurudi nyuma.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Abubakari Kunenge alieleza, Global Fund wanasaidiana na Serikali ya Rais Samia Suluh Hassan katika kuboresha huduma za afya.

Alieleza ,mkoa wa Pwani umefanikiwa kusogeza huduma za afya karibu na jamii ili kuwaondolea kero wananchi.

"Tunashukuru Waziri kwa ujio wako na mgeni katika mkoa wetu kujionea jinsia tunavyofanya kazi ya kutoa huduma ya afya kwa jamii"alisema Kunenge.

Mkurugenzi huyo wa Global Fund , Sand alifafanua Mfuko huo una utaendelea kushirikiana na nchi ya Tanzania na Kuna mahusiano ya kipindi kirefu ,na aliwahakikishia kuendelea kusaidia ili kuboresha sekta ya afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...