Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza katika mkutano na Waandishi kwenye mkutano uliofanyika leo asubuhi Kibaha Mkoani Pwani

Na Khadija Kalili, Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge ametangaza tarehe rasmi itakayofanyika Wiki ya Uwekezaji Pwani ambapo maonyesho hayo yatatoa taswira ya wepesi na urahisi kwa wawekezaji kuwekeza ndani ya Mkoa wa Pwani.

Akizunzungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uluofanyika leo Septemba 9 kwenye Ukumbi wa mikutano uliopo Wilayani Kibaha Mkoani hapa amesema kuwa hivi sasa baadhi ya wawekezaji wamekua wakiishi ndani ya Mkoa kutokana na kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi.

Amesema kuwa maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu ambapo yatafanyika kwenye viwanj vya stendi ya zamani ya Mailimoja Kibaha.

Amesema kuwa Mkoa tayari umefanya maandalizi ya kutosha pia wanatarajia kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa na Kiongozi mkubwa kutoka serikalini.

"Wiki ya Biashara na Uwekezaji imepangwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 6 2022 na inatarajiwa kushirikisha washiriki 520 na kukadiriwa kupata watembeleaji 15,000." amesema RC Kunenge.

Amesema kuwa maonyesho haya yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na SIDO ambapo pia itahusisha Kanda ya Kusini Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani yote itahusika kwenye maonyesho hayo" amesema RC Kunenge.

Maonyesho haya yanafanyika kwa mara ya tatu ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika 2018 na 2019 " amesema RC Kunenge.

RC Kunenge amesema amesema kuwa tukio hili ni muendelezo kwa kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais wa wetu wa Jamuburi ya Muungano Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa katika mstari wa mbele katika kuvutia wawekezaji na kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini pamoja na kuboresha uchumi wa nchi yetu" amesema RC Kunenge

Amesema kuwa mbali ya viwanda, ufugaji, uwindaji wa kibiashara , utalii , pia Mkoa wa Pwani una madini mengi bila kusahau fursa ya uvuvi hivyo wananchi na wazawa wa ndani na nje ya nchi wote wanakaribishwa' amesema RC Kunenge na kuongeza kuwa Mkoa una viwanda zaidi ya 1460 huku idadi ha viwanda vikubwa ni 90

Afisa Biashara Mwandamizi (TANTRADE) Rehema Akida amesema nafasi kwa wanaopenda kushiriki kwenye maonesho hayo zimebaki chache hivyo wachangamkie fursa ili waweze kuonyesha bidhaa zao " amesema Rehema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...