NA YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO
Afisa mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Kelvin Methew Mnali alidai idara ya mazingira ni idara mtambuka hivyo kupitia mazingira yaliyopo wilayani Namtumbo kuwa ni wezeshi kwa wawekezaji wa aina yoyote.
Mnali alisema mazingira ya wilaya ya Namtumbo ni wezeshi kwa kilimo cha aina yoyote kutokana hali ya hewa iliyopo inaruhusu wawekezaji kuanzisha kilimo cha mazao ya chakula na biashara kwa wingi kutokana na kuwepo kwa ardhi nzuri ya kilimo pamoja na kuwepo kwa hali nzuri ya hewa ya kuwezesha kuzalisha mazao hayo.
Aidha Mnali alisema wilaya ya Namtumbo imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali kadiri ya ripoti ya utafiti uliofanywa na unaoendelea kufanywa na kampuni au vikundi vilivyopewa leseni za kufanya utafiti katika wilaya ya Namtumbo ,kampuni au vikundi hivyo vimeonesha kuwepo kwa madini mbalimbali katika maeneo mengi lakini maeneo hayo yamekosa uwekezaji na kushindwa kuendelezwa alisema afisa mazingira huyo.
Kampuni au vikundi vilivyopewa leseni ya kufanya utafiti katika wilaya ya Namtumbo wamebaini kuwepo kwa madini ya beryllium,guartz,amozonite,spodumene,mica,felisper,manganese ,nobium ,titanium,moonstone na tantalite.
Mnali alitaja Madini mengine kuwa ni Dhahabu,Aguamarine,iron,coal,topaz na phosphate na kudai kuwa sekta hiyo inahitaji uwekezaji ili kuwekeza katika sekta hiyo ili kuwawezesha wananchi na serikali kuendeleza maeneo hayo.
Wilaya ya Namtumbo imebarikiwa kuwa na misitu minene ya asili ,hifadhi za jamii na mbuga za wanyama za Selous na Nyerere hali inayoifanya wilaya hiyo kuwa na maeneo makubwa yanayohitaji uwekezaji ili kuyaendeleza maeneo hayo.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ni moja kati ya Halmashauri nane zinazopatikana mkoa wa Ruvuma ambayo inahitaji kampuni ,watu binafsi kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuiwezesha Halmashauri hiyo kuendeleza fursa zake zilizopo ili kuiwezesha serikali kupata mapato ili kuwaletea wananchi wake maendeleo
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa upande wa kaskazini imepakana na mkoa wa Ruvuma,kusini imepakana na nchi ya Msumbiji,Mashariki imepakana na wilaya ya Tunduru na magharibi imepakana na wilaya ya Songea ambapo wilaya ya Namtumbo imesheheni kuwepo kwa fursa za uwekezaji kati ya Halmashauri hizo nane za mkoa wa Ruvuma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...