Na Mwandishi Wetu,Michuzi
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam Godwin Gondwe leo Oktoba 26,mwaka 2022 amezindua ‘App’ mpya ambayo itafahamika kwa jina la Wese itakayokuwa ikiwezesha madereva kununua mafuta na kulipa baadae bila riba wala kamisheni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa App ya Wese, Gondwe ameeleza kwamba Wese ni jukwaa la kifedha na biashara ambalo litakuwa linaunganisha sekta ya uchukuzi, petroli na fedha.
"Huduma hii inatarajiwa kufanyiwa majaribio katika Mkoa wa Dar es Salaam mwezi ujao , ikilenga kuwawezesha madereva wote wa magari makubwa, madogo, daladala, pikipiki na bajaji na wafanyabiashara kupata huduma ya mafuta kwa unafuu zaidi,"amesema.
Amoengeza na kuzinduliwa kwa ‘App’ hiyo kunakwenda kuibua fursa kwa vijana wanaojihusisha na shughuli za usafirishaji.Aidha mfumo wa kieletroniki utaenda kubadili maisha ya vijana na kuwajenga katika nidhamu ya kutunza fedha na kukua kibiashara.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mfumo wa Wese Francis Ekeng raia wa Nigeria amesema mfumo huo unafanana na mfumo kama wa taxi mtandao, ambao muhusika atalazimika kupakua ‘app’ hiyo kwenye simu yake ya kiganjani na kujisajili.
“Mtu akishajisaji atakuwa na uwezo wa kujaza mafuta ya gharama yoyote anayotaka katika kituo chochote cha mafuta nchi nzima, ila atatakiwa kulipa kabla ya saa sita usiku,” amesema.
Akifafanua zaidi anasema iwapo dereva atashindwa kulipa deni kwa wakati, atapigwa faini na iwapo atalipa kwa wakati atapata fursa ya kukidhi vigezo vya kukopesheka zaidi kutokana na uaminifu.
“Kila dereva anapochukua mafuta na kulipa bila kupata adhabu au kushindwa, pointi inatolewa ambayo inamjengea sifa yake ya kukopesheka zaidi,” amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe (kulia) akisalimiana na Mwakilishi wa Mfumo wa Wese Francis Ekeng raia wa Nigeria leo Oktoba 26,mwaka 2022 Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa ‘App’ mpya ambayo itafahamika kwa jina la Wese leo Oktoba 26,mwaka 2022 Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wa Mafuta.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Godwin Gondwe akita katika picha za patoja na wanadau wa Mafuta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...