Na Mwandishi Wetu, Ufaransa

KUTOKANA  na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, bidhaa nyingi na zenye ubora kutoka Tanzania zimeanza kupata masoko katika nchi za Ulaya. 

Hayo ni maparachichi kutoka Tanzania ambayo yanauzwa katika "supermarket" kubwa iitwayo Carrefour mjini Paris, Ufaransa. Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa unatoa mwito kwa wakulima na wafanyabiashara nchini Tanzania waandelee kuzalisha  kwa wingi bidhaa zenye ubora kwa ajili ya masoko ya nchi za Ufaransa, Uhispania na Ureno.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa umeeleza kwamba "Tunawaomba wakulima na wafanyabiashara wa aina mbalimbali kuzalisha kwa wingi bidha nyingi na zenye ubora, soko katika nchi za Ulaya ni kubwa, hivyo ni wakati wetu kutumia soko hilo kuuza bidhaa za kutoka nyumbani."ni 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...