Na Mwandishi wetu, Simanjiro

BILIONEA Saniniu Laizer mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyosimamia miradi mingi ya maendeleo.

Bilionea Laizer ameyasema hayo jana wakati akizungumza na maelfu ya wakereketwa, wanachama wa CCM na wananchi mbalimbali waliomsindikiza mdogo wake Kiria Laizer ambaye ni Mwenyekiti mpya wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro.

Amesema Rais Samia amefanikisha miradi mingi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara hivyo watanzania waendelee kumuunga mkono.

“Kwa dhati ya moyo wangu nampongeza mama yetu mpendwa Rais Samia kwa namna ambavyo anaiongoza Serikali ya awamu ya sita na kufanikisha miradi ya mbalimbali ya maendeleo,” amesema Bilionea Laizer.

Amesema japokuwa yeye siyo mwanasiasa ila kupitia miradi ya maendeleo inayofanyika maeneo mbalimbali nchini anampongeza sana Rais Samia kwa hatua hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro, Kiria Laizer akizungumza kwenye mapokezi hayo huku akitoa machozi amemshukuru kaka yake Bilionea Laizer kwa namna alivyomlea hadi kufikia hatua hiyo.

“Baba yangu mzazi amefariki dunia nikiwa mdogo na mama yangu pia akafariki, lakini kaka yangu Bilionea Laizer akawa ndiyo mzazi wangu na akanilea kwa maadili mema na kunisomesha hadi mimi kufikia hatua hii ya kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro namshukuru sana,” amesema Kiria na kushindwa kuendelea kuzungumza kutokana na machozi kumtoka.
Bilionea Saniniu Laizer mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Kiria Laizer (kushoto) kwenye mapokezi yaliyofanyika Kata ya Naisinyai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...