Adeladius Makwega MAKOLE
Siku moja nilipigiwa simu na ndugu yangu mmoja niliyesoma naye sekondari, akiniuliza ehe mwanakwetu upo Dodoma? Nilimjibu kuwa nipo Dodoma lakini leo sipo kidogo Idodomia nimesafiri kidogo. Akaniuliza upo wapi? Nilimjibu kuwa nipo Lushoto Tanga kuna shughuli ya mwanagu.
Ndugu yangu huyu aliniuliza ni shughuli gani hiyo mwanakwetu mbona hatualikani? Unaoozesha? Nilimjibu hapana bali mwanagu mmoja anapata Komuniyo ya kwanza. Ndugu huyu ambaye ni muisilamu tangu tunasoma akacheka sana, alafu akasema mwanakwetu bado unaendeleza TYCS-MAPENDO ? Nikamjibu ndiyo.
Kwa msomaji wangu ambaye hafahamu TYCS ni Tanzania Young Catholic Students yaani Umoja wa Vijana Wanafunzi wa Kikatoliki Tanzania, Huyu jamaa tulisoma naye anakumbuka mambo shuleni namna mwanakwetu nilivyokuwa katika umoja huo wa kiroho na ndiyo maana aliuliza hilo.
Mazungumzo na ndugu yangu huyu yalikuwa marefu sana, binafsi nafahamau pahala anapofanya kazi ndugu huyu nikamuuliza nayeye bado anafanya kazi kule kule? Akanjijibu ndiyo na hapa anapoongea anapita Mji wa Serikali, alitamani kuniona tuongee kidogo. Nikamjibu leo hii kwa bahati mbaya sipo huko .
Nikamuuliza na yeye anatokea wapi kwenda wapi ? Akanijibu kuwa anatokea hospitali mojawapo kubwa jijini Dodoma alimpeleka mama yake mzazi kutibiwa. Nikamuuliza kama alipata matibabu, ajibu alipata. Nikampa pole ya ugonjwa wa mama yake huyo. Akaniambia anahangaika mno na matibabu ya mama yake kwa kuwa wao kazini hawana Bima ya Afya.
Nikamuuliza mbona watumishi wote wa umma wana bima ya afya ? Akanijibu kuwa wao wanatibiwa kwa utaratibu wa kwenda hospitali za taasisi zao. Nikauliza kweli? Akajibu kweli na kama angekuwa na bima ya afya mama yakey angeshatibiwa lakini hapo kama yeye, mke , mtoto au mtegemezi wake anahitaji matibabu nje ya hospitali hizo wanapaswa kuomba kibali cha kutibiwa hospitali zilizo nje ya taasisi yao au vingenevyo labda itoke pesa ya mfukoni mwako.
Mwanakwetu ndugu yangu huyu mabegani mwake kachafuka sana na msomaji wangu usione gere, shuleni alikuwa na akili sana ndugu huyu. Nikamwambia kaka kwanini msiombe kubalishiwa huo utaratibu? Ndugu huyu alijibu kuwa mwanakwetu huku hakuna vyama vya wafanyakazi, ukileta siasa utanachaguliwa balozi, alaa ubalozi wa nyumba kumi kumi? Niliuliza, akacheka sana alafu akajibu ndiyo.Nikasema hongereni.
Mwanakwetu simu hiyo ilikata na mimi kuendelea na maandalizi ya Komuniyo ya mwanangu huko Lushoto. Nikiwa katika maandalizi hayo nikajiuliza kama ndugu huyu amepatwa na ugonjwa huku wilayani mpaka kuifikia hiyo hospitali yao bado ataendelea kuwa salama?
Mathalani mwanangu ni anafanya kazi huko alafu akapata ajali natambua atatibiwa klwa dharula lakini matibabu yake yatakuwa kwa hisani kwanini wasiwe na bima ya afya? Nilijiuliza.
Binafsi nikaona kuna umuhimu mkubwa hawa ndugu kuwapa bima ya afya kila mmoja wao,wenza wao, watoto wao na wategemezi wao ili watibiwe katika zahanati , kituo cha afya hospitali ya wilaya, hospitali ya mkoa au ya rufaa.
Mwanakwetu kwa nini siku yaleo nasimulia mawasiliano haya ya simu? Oktoba pili, 2022 nilipoona uteuzi wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa kuwa Mheshimiwa Innocent Bashungwa nikamkumbuka ndugu yule siku ile na komuniyo ya kwanza ya mwanagu.
Nikasema kwa kuwa sasa wizara hii imepata waziri mpya aibebe hii hoja, iwe kama ya mtoto wake wa kumzaa na namna anavyowezatibiwa ili kuhakikisha ndugu hawa wanakuwa na bima za afya kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma.
Binafsi ninamfahamu mheshimiwa Innocent Bashungwa akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na baadaye akawa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, akiwa katika wizara hizi ndugu huyu alijitahidi mno kujifunza kujenga ujirani baina ya viongozi na watumishi wa chini huku akifanya nao vikao vingi na kuyatatua mambo mengi ya watumishi wa chini. Hoja juu ya uwaziri wake akiwa TAMISEMI ninasema wazi Mheshimiwa Bashungwa hakufanya vizuri, bado wizara hii kuna changamoto nyingi hazijafanyiwa kazi, afadhali wakati alipokuwapo Mheshimiwa Seleiman Jaffo kidogo alijitahidi.
Mheshimiwa Bashungwa akiwa WHUSM na WUSM Kazi yake aliifanya vizuri sana akishirikiana kwa karibu na Manaibu Waziri wake wa wakati kwanza ndugu yangu Abdalla Ulega aliyekaa naye kidogo sana alafu dada yangu Pauline Gekul walifanya nae kazi zuri kwa ushirikiano wa karibu ambao macho yangu hayajajaliwa kuuona tena.
Binafsi ninaamini Mheshimiwa Bashungwa anaweza kuifanya kazi hiyo vizuri sana kwa kuwa tayari ameshajifunza usikivu kwa wale walio chini yake.Wizara hii inahitaji umakini wa kuwasikiliza wale walio chini siyo sawa na TAMISEMI yenye mkululu wa mambo.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...