Na Mwandishi Wetu ,Michuzi Tv
MAKANDARASI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kulalamika badala yake waweke juhudi ili wapate kazi kubwa zinazotangazwa ndani ya nje nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB), Mhandisi Consolata Ngibwa, alipofungua mafunzo ya siku tatu ya wakandarasi yanayohusu usimamizi wa biashara na fedha.
Ngimbwa alisema dunia imebadilika na kwamba wakandarasi, lazima waache tabia ya kulalamika na badala yake wahakikishe wanaweka juhudi katika kuomba kazi na wakizipata wazifanye kwa uaminifu.
"Kuna fursa nyingi nchini, lakini kama makandarasi watabaki kulalamika hawawezi kuzipata na wataendelea kulalamika siku zote," alisema
"Yaani ni sawa ukimsalimia mtu umeamkaje, kila siku yeye utasikia mguu unauma, mara mbavu zinauma, yaani yeye kila siku ni kulalamika tu na sisi tusiwe hivyo, badala yake tuwe na uthubutu," alisema
Aliwataka makandarasi hao kutumia mafunzo hayo yanayohusu kuwajengea uwezo wa usimamizi wa biashara na fedha katika miradi, kujifunza na kufahamu mambo yanayohusu kazi zao.
Kwa upande wake, Msajili Msaizidi wa Utafiti na Maendeleo wa CRB, David Jere alisema ili wakandarasi waweze kupiga hatu ni lazima wajue kazi wanazoomba na wanazozifanya.
Alisema kama mkandarasi hana mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha itakuwa ngumu kwake kupiga hatua hata kama atafanya kazi kwa muda mrefu.
Aliongeza kuwa mafunzo ya usimamizi wa fedha na baosjara yatawapa uelewa wakandarasi Ili kuwawezesha kutekeleza kazi zao Kwa weledi.
Kuhusu makandarasi kuungana na kuomba kazi kubwa zinazotangazwa, Jere alisema wanatakiwa kusaini mkataba mzuri utakaowalinda Ili wasigombane wakati wa utekekezaji na baada ya kumaliza mradi.
Alisema makandarasi wengi wanashindwa kuungana kutokana na kuhofia kugombana kwa kuwa kila mtu anakuwa na kampuni yake na hivyo kufanya kazi pamoja inakuwa ngumu.
Akitoa mafunzo kwa wakandarasi hao, Dk. Darling Mutalemwa, alisema.yanalenga kuwajengea uwezo kuhusu usimamizi wa biashara zao.
Alisema kwa sasa mazingira ya kazi yamebadilika hivyo ni lazima wakandarasi wafahamu hilo na kukubali kujifunza.
Aliongeza kuwa mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha na biashara ni muhimu na kwamba washiriki pia watapata fursa ya kujua shughuli mbalimbali zinaozfanywa na serikalk na namna gani anaweza kuomba kazi zinazotangazwa.
Mmoja wa wakandarasi kutoka mkoani Arusha, Daniel Kweka akizungumza katika mafunzo hayo, aliwataka wenzake kuacha tabia ya kuchukua malipo ya kwanza ya kazi (advance) na kuzituma kuoa mke badala ya kuzifanyia kazi.
Alisema ili mkandarasi yoyote awe mdogo ama mkubwa aweze kupiga hatua ni lazima awe na nidhamu ya fedha anazolipwa Kwa ajili ya kazi.
"CRB imenisaidia sana, huyu mama Ngimbwa tumeenda naye mpaka nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza wenzetu wanafanyaje kazi katika sekta hii," alisema Kweka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo makandarasi wa ndani kuhusu usimamizi bora wa biashara na fedha yanayoendelea jijini Mwanza, ambayo yameandaliwa na bodi.Makandarasi wanaoshiriki mafunzo ya siku tatu kuhusu usimamizi wa fedha na biashara jijini Mwanza wakifuatilia mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...