Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv
YEMCO VIKOBA kwakushirikiana na Mfuko wa Uwekezaji Tanzania UTT ikiwemo Kampuni ya simu ya Vodocam zimeungana pamoja kuahakikisha fedha za vikundi vya ujasiriamali vinawezeshwa kuhifadhi fedha zao kwa kupitia M-COBA kwa ajili ya kukuza Mitaji yao kwa maeneeleo endelevu.
Akizunguza wakati wa maadhimisho ya siku ya YEMCO VIKOBA iliyofanyika Mkoani Dar es Salaam Rais wa YEMCO VIKOBA nchini Mohamed Basanga asema hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa wanavikundi kuweka fedha zao kwa tija.
Aidha Rais huyo ameeleza namna walivyojipanga kuhakikisha Elimu ya Vicoba inafikiwa wananchi wengi zaidi katika maeneo mengi ya nchi huku mwakilishi wa Mfuko wa Uwekezaji Tanzania UTT AMIS akisema Elimu ya uwekezaji kwa Wananchi wengi ni changamoto hivyo kuwepo Kwa mashirikiano hayo kuwatawasadia wajasiriamali kuwekeza kwa tija.
Rais wa YEMCO VIKOBA nchini,Mohamed Basanga (katikati) Akizungumza na waashidhi wa habari namana ya kujiunga na vikoba na namana utakavyo kapata faida baada ya ukijiunga jana katika ukumbi wa Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.
Waandi wa habari wakimsikiliza Rais wa YEMCO VIKOBA nchini,Mohamed Basanga
Mtaalamu wa Lishe,Peter Twete akiwaonesha waandishi wa habari vitu mbalimbali vinavyohusiana na lishe bora jana katika ukumbi wa Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...