Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na mmoja wa watumishi wa Wizara alipowasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine.WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.), Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara.

Dkt. Tax ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Oktoba 2022 na kuapishwa tarehe 03 Oktoba 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Tax amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula baada ya Mhe. Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri.

Akizungumza baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Mhe Dkt. Tax amesema atashirikiana na watumishi wote wa Wizara katika kila ngazi ili kuhakikisha malengo ya Wizara yanatekelezwa kikamilifu.

“Nipo tayari kufanya kazi na nyinyi, na kujifunza kutoka kwenu ili kutekeleza majukumu yangu….. Taasisi yoyote ili iweze kufanikiwa lazima ifanye kazi kwa pamoja na kuwa na ushirikiano,” amesema Dkt. Tax.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokelewa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipowasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakimsikilza Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine alipokuwa akimkaribisha Dkt. Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara na baadhi ya watumishi katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...