Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Sinach Joseph Egbu anatarajia kuongoza jukwaa la Festival of Praise linalotarajia kufanyika Oktoba 16 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Tanzania Daima muandaaji wa tamasha hilo, mwimbaji maarufu hapa nchini, John Lissu alisema umahiri wa Sinach utafanikisha ujumbe wa neno la Mungu kuwafikia watanzania wote kupitia tungo zake na waimbaji wengine wa hapa nchini.

Lissu alisema Sinach atapanda jukwaani na wimbo wake uliokamata anga la muziki wa Injili duniani wa ‘Way Maker’ uliotazamwa na mashabiki zaidi ya milioni 200.

Lissu alisema waimbaji wa hapa nchini watakaomsindikiza mwimbaji huyo ni pamoja Nay Eye, Christina Shusho, Ambwene Mwasongwe, Pasta EPA, Kwaya ya Kanisa la Moravian, Ruach Worship Team (Kenya) na Kwaya ya Gospel Winners.

Aidha Lissu alitoa wito kwa waamini wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo ni mojawapo ya matukio muhimu ya kusifu na kuabudu yanayofanyika hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...