Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini Mha. Lorivii Longidu, akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt.Mussa Chacha, mara baada ya semina.
Baadhi ya Wanafunzi wa kada ya umeme kutoka chuo cha ufundi Arusha, wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Lorivii Longidu, akizungumza wakati semina ya mafundi umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha.
Baadhi ya Wanafunzi wa kada ya umeme kutoka chuo cha ufundi Arusha, wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
EWURA Kanda ya Kaskazini, Tar. 20/10/2022 imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa kada ya umeme katika chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kuhusu utaratibu wa uombaji wa leseni za ufungaji wa mifumo ya umeme.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Mha. Lorivii Long’idu, ameeleza kuwa, elimu hiyo itawasaidia wanafunzi hao, kuelewa miongozo mbalimbali ikiwamo sheria na kanuni katika kazi za umeme.
“Elimu hii imelenga kuwaandaa wanafunzi hawa pindi wanapomaliza masomo yao, kuomba leseni ya ufundi umeme EWURA, ili wakafanye kazi kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha sheria ya umeme, inayotaka mtu yeyote kuwa na leseni kutoka EWURA, ndipo afanye shughuli za ufungaji wa mifumo ya umeme”
Katika semina hiyo, EWURA imeeleza mahitaji muhimu wakati wa maombi ya leseni za ufungaji wa mifumo ya umeme.
Vilevile uchanganuzi wa madaraja ya leseni za ufundi umeme na masharti ulifafanuliwa kama ilivyoainishwa katika Kanuni za ufungaji wa mifumo ya umeme za mwaka 2022, zinazopatikana katika tovuti ya EWURA www.ewura.go.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...