_6.jpg)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Lameck Hiliyai akikata utepe kuashiria uzinduzi wa PumaGas leo Oktoba 20, 2022 jijini Dar es Salaam akishuhudiwa na Wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara wa wadogo na wakubwa.
_8.jpg)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Lameck Hiliyai akizungumza na wafanyabiashara wa gesi leo Oktoba 20, 2022 wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa wafanyabiashara hao.
.jpg)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Lameck Hiliyai akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Puma Gas leo Oktoba 20, 2022 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Lameck Hiliyai akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Puma Energy Tanzania leo Oktoba 20, 2022 jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua mafunzo kwa wafanyakazi wadogo na wakubwa.
KATIKA kuendelea utunzaji wa Mazingira kampuni ya nishati ya Puma Tanzania Limited kuanza kuuza gesi katika Uzazo tofauti tofauti hapa nchini.
Kampuni hiyo pamoja na kuuza gesi watatumia Aplikesheni ya kiubunifu ambayo ni 'PumaGas' ambapo mtumiaji akitaka gesi hiyo ataitumia wakati wa kununua au kutoa taarifa pale anapohitaji gesi nyingine.
Akizungumza wakati wa kuzindua gesi hiyo leo Oktoba 20, 2022 jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Lameck Hiliyai amesema kuwa uzinduzi huo umeambatana na mafunzo kwa wafanyabiashara wa jijini Dar es Salaam ili kuonyesha jinsi inavyoleta urahisi kwa watumiaji na wasambazaji, huku pia ikihudumia jamii kubwa zaidi kwa kwa kurahisisha upatikanaji na kuboresha usalama.
Amesema kuwa Wanaunga juhudi za serikali katika kukuza teknolojia, usalama wa gesi kwa Mtumiaji pamoja na utunzaji wa mazingira ili kufanikisha malengo ya Nchi kwa Ujumla.
"Serikali imeona ongezeko kubwa la matumizi ya Liquelified Petrolium Gas (LPG) katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, sekta hiyo imeshuhudia ukuaji wa uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kwa wastani wa zaidi ya 20% mwaka hadi mwaka kuanzia 2017 hadi 2021. Ni dhahiri matumizi ya LPG nchini Tanzania pia yameongezeka, kutokana na muendelezo wa maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania na kuongezeka kwa uelewa wa LPG kama njia bora zaidi ukilinganisha na kuni au mkaa, inatarajiwa kuendelea kukua hadi viwango vya juu zaidi mijini na vijijini. Kwa kuwa PumaGas sasa iko sokoni, itaunga mkono azma ya serikali ya Tanzania ya kuongeza matumizi ya LPG kote nchini." Amesema Hiliyai
Amesema, "Tanzania inawakilisha soko muhimu la PumaGas inaakisi dhamira yetu kuboresha shughuli za Upishi kwa usafi kote nchini." Ameeleza
Akizungumzia kuhusu Aplikesheni ya 'PumaGas' amesema ni Game Changer kwa mtu yeyote ambaye anataka kurahisisha maisha yake. Aplikesheni imeundwa ili kuleta urahisi kwa watumiaji wa gesi ya kupikia. Wateja wanaweza kuagiza PumaGas moja kwa moja kupitia simu janja ya mkononi kwa njia ya USSD au kwa kupakua Aplikesheni ya PumaGas ili kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kuliko hapo awali.
Amesema wazo hilo la bunifu lilitokana na azma ya kupata suluhisho ambalo litawawezesha watumiaji wa LPG kupata gesi ya kupikia kwa urahisi mahali walipo, kwa wakati na vile vile kuifikisha nyumbani bila malipo ya usafiri, kwa kubofya kitufe tu.
"Tumehakikisha tunakuwa na wafanyabiashara wakubwa katika mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudumia maeneo mbalimbali ya jiji hili na baadaye mwaka huu mtandao wetu wa wafanyabiashara utakua mikoa mingi zaidi ili kuhudumia wateja kote nchini.” Amesema
Kwa Upande wa Afisa Msaidizi wa Malaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA), Catherine Ochido amesema kuwa watahakikisha watumiaji wa gesi wanapata uelewa wa namna sahihi ya utumiaji wa gesi bila kupata madhara.
Pia amewapongeza kampuni ya Puma kwa Kuuza gesi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuwapa urahisi watumiaji wa bidhaa za Puma kwa kutumia aplikesheni ya Puma App.
Meneja Masoko wa Puma Energy Tanzania, Lucas Meene amesema kuwa Kampuni hiyo imejikita zaidi katika usalama wa bidhaa zao kwa watumiaji.
"Puma Energy inaunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha Nishati Mbadala, kwa Rangi yake ya kijani inawakilisha mazingira yetu, na kila wakati inatukumbusha kulinda mazingira yetu." Amesema Meena.
Akizungumzia kuhusu Vipimo vya gesi ya Puma Afisa Kutoka wakala wa Vipimo Tanzania, Grace Kulengwa amesema kuwa kampuni ya Puma wamezingatia Vigezo vya Vipimo kwani wamemjali mtanzania wa kawaida mpaka mtanzania mwenye uwezo mkubwa wa kutumia gesi.
Amewaasa wafanyabiashara wa Puma Gesi kupima gesi pale inapofika katika duka na kupima pale ambao wanampelekea mteja wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...