Na Jane Edward, Arusha
Takribani wakandarasi 18 waliosaini mikataba ya kutengeneza miundo mbinu ya barabara na madaraja, wametakiwa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia muda ambapo kwa wale watakaoenda kinyume na taratibu walizojiwekea kushughulikiwa.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela wakati wa zoezi la utiaji Saini kwa wakandarasi wa barabara na madaraja.
Mongela amesema Mikataba hiyo ina thamani ya sh,bilioni 4 kati ya Wakala wa barabara vijijini na Mijini ( TARURA) na wakandarasi 18 ,huku fedha hizo zikiwa ni fedha za nyongeza zilizotokana na tozo.
" wakandarasi mnatakiwa kufanya kazi kwa kufuata miongozo iliyopo kwenye mikataba hiyo , kwa kutekeleza mradi kwa viwango na kuepuka ucheleweshaji na kutokidhi ubora wa mradi"Alisema Mongela
Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha mhandisi Laynas Sanya alisema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 walipatiwa jumla ya fedha za matengenezo ya barabara zaidi ya bilioni 18 kwa awamu ya pili na katika awamu ya kwanza mikataba 34 ilisainiwa yenye thamani ya bilioni 14.
Aidha awamu ya pili ya utiaji saini jumla ya mikataba 18 yenye thamani ya zaidi ya sh,bilioni 4 imesainiwa na wakandarasi mbalimbali wazawa watakaotekeleza miradi ya miezi sita kwa kiwango na ubora unaotakiwa.
"Mikataba hii tumesaini ikiwa ni kufuata mwongozo wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ambaye alielekeza mikataba yote isainiwe hadharani bila usiri"Alisema meneja
Akifafanua zaidi amesema wakati wa utekelezaji wa miradi ya barabara mwongozo wa serikali unawataka pia kuweka taa za barabarani jambo ambalo alisisitiza wameanza kulitekeleza.
Hata hivyo alisisitiza kuwa Tarura itahakikisha inawasimamia wakandarasi hao ili miradi hiyo inayotengenezwa iweze kukamilika kwa wakati .
.jpeg)
Kulia aliyevaa miwani ni meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha Laynas Sanya akishuhudia zoezi la utiaji saini kwa wakandarasi hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...