Na Khadija Kalili
MKURUGENZI Mtendaji Mradi wa 'Mbakiamturi Rice Project' Hamisi Kambanga amesema kuwa hivi sasa wanakabiliana na shida ya ukosefu wa miundombinu ya umwagiliaji hivyo wameiomba serikali kuwawezesha ili waepukane na kilimo cha kutegemea mvua kwa sababu wakilima kilimo cha umwagiliaji watakuwa na uhakika w kuvuna na kuzalisha mpunga mara mbili kwa mwaka.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa endapo wataendelea kulima kilimo cha kutegemea mvua hawataweza kujikwamua na umasikin kwa sababu kilimo kinakuwa hakina uhakika wa kuvuna endapo mvua isiponyesha . Amesema kuwa mitaji inaweza kupotea kwa sababu mazao lazima yatanyauka kwahiyo ili kuweza kupata suluhu ya changamoto hii ni kuwawezesha kupata miundombinu ya umwagiliaji inayokadiriwa kugharimu kiasi cha fedha Bil.3 kiasi ambacho kitahitajika katika awamu ya kwanza ya umwagiliaji kwa kumwagilia hekari 8,800.
Mbakiamturi Rice Project ni wawekezaji vijana katika kilimo cha kisasa cha Mpunga waliowekeza kwenye mashamba yaliyopo Wilayani Kibiti Mkoani Pwani. "Tunamuomba Waziri wa Wizara ya Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe afike katika mashamba yetu na kuweza kuona namna atakavyoweza kututatulia changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo ikiwemo miundombinu mibovu ya namna ya ufikaji mashambani" amesema Kambanga.
Mkurugenzi huyo wa Mbakiamturi Rice Project amesema hayo hivi karibuni alipozungumza na kubainisha kuwa licha ya wamegubikwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa barabara, maji mawasiliano ya mtandao.
"Ukiwa kijijini huwezi kufanya jambo lako kwa sababu namna ya ufikaji mjini kufuata mahitaji muhimu nauli kwenda na kurudi inagharimu Sh. 50,000 kwa njia ya usafiri wa pikipiki jambo ambalo limekua changamoto kubwa tunazokabiliana nazo , pia hakuna mitandao (Internet) tunahitaji mitandao kwa sababu hivi sasa dunia ni kijiji pia huduma zote zinapatikana kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mbakiamturi Rice Project, Hamisi.Kambanga mradi huo uliopo Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...