Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MWENYEKITI mpya wa Jumuiya ya wazazi CCM ,Kibaha Mjini, Yahaya Mtonda ameweka bayana mikakati yake manne ikiwa ni pamoja na kubuni vitega uchumi vipya na kuunda vikundi vya kujiinua kiuchumi ndani ya Jumuiya ili kuondokana na utegemezi.

Aidha kuratibu semina elekezi za mafunzo kuanzia ngazi ya tawi hadi wilaya ili viongozi wapate uelewa sambamba na kujenga mahusiano mazuri baina ya Jumuiya , Chama na Serikali.

Akitoa msimamo wake huo, baada ya kuibuka kidedea nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo 2022-2027 ,katika mkutano mkuu wa Jumuiya ya wazazi wilayani humo, uliokuwa na agenda kuu ya uchaguzi ,Mtonda alisema pia kuwapa uwezo wa vitendea kazi kama kompyuta ili kuwepo na urahisi wa kazi na usiri kwenye majukumu yao.

Alisisitiza kwamba, kura 159 alizopata dhidi ya wenzake wawili ni deni ambalo ataulizwa baada ya kipindi cha miaka mitano.

"Nashukuru mkutano mkuu kwa kunichagua ,nimeweka historia ,"najua wapo ambao hawakunikubali Ila namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa uongozi huu,najua ni DENI KUBWA AMBALO NASTAHILI KULILIPA KWA AHADI NILIYOITOA KWENU, naahidi kuwatumikia ,kuwaunganisha na kushirikiana kwa umoja ili kusimama imara"

"Kazi ya kuwaunganisha wanachama na viongozi baada ya makundi ya uchaguzi ni kubwa Lakini mnapaswa kuungana ili kufikia mikakati niliyojiwekea, !"Mtonda alieleza.

Awali akisoma matokeo , msimamizi wa uchaguzi huo, Katibu wa Jumuiya ya wazazi Bagamoyo Aeshi Rajabu alisema, Mtonda ameshinda kwa kura 159 ,Simon Kushoka Luhende kura 81 na Mariaconsolata Mvula kura 63.

Nafasi ya Mjumbe mkutano mkuu Wazazi Taifa alishinda Sara Peter Uledi kwa kura 178 na nafasi Mjumbe mkutano mkuu wazazi mkoa ni Hawa Kadibo 110 .

Aeshi alisema , nafasi ya uwakilishi kwenda Vijana amekosekana kutokana na kukosa mtu mwenye sifa na vigezo vya umri wa kijana kwani hakuna aliyefikia umri ,hivyo nafasi hiyo itachaguliwa baadae.

Nae Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mjini Kibaha Sharon Tulliy alieleza ni taratibu kwa Chama kufanya chaguzi zake kila baada ya miaka mitano ,"changamoto haziwezi kukosekana ila anamshukuru changamoto zilizokuwepo zilikuwa ndogo ambazo zimeweza kutatulika na uchaguzi umefanyika salama.

Alisema viongozi wote waliogombea walikuwa bora Ila wanachama wametimiza wajibu wao kuchagua viongozi wanaowahitaji.

Sharon alieleza ,anaimani na waliochaguliwa Kuwa wanakwenda kuivusha Jumuiya na kuwataka kuwa wamoja kusimamia Jumuiya ili ipige hatua ya kimaendeleo.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...