SERIKALI nchi imesema kuwa itahakikisha kuwa wasanii nchini wanatimiza ndoto zao na kuitangaza nchi kimataifa.
Hayo yamesemwa Oktoba 15, 2022 na Dkt. Ishongoma Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wakati wa uzinduzi wa vazi la Tribe Called Afrika linaloitambulisha Tanzania na Afrika Dunia lilibuniwa na Mwanamitindo wa Kitanzania Dominic Godfrey akishirikiana kulitangaza na Mwanamitindo na Msanii wa film nchinu uengereza Oris Erhuero.
Amesema kuwa sekta ya ubunifu wa mavazi inazidi kuitangaza nchi kimataifa.
"Sisi kama Serikali tunalojukumu la kuhakikisha sekta hii inasonga mbele"
Amesema kuwa Serikli inaanzisha mfuko maalum kwa ajili ya wasanii wote ili wapate fursa ya kukopa "mtakopa bila riba ili muweze kurejesha mikopo na wengine wapate fursa ya kukopa itasaidia kuinua wasanii wetu".
Naye Dk Kedmon Mapana Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa (Basata), amelisifu vazi la ubunifu liliobuniwa na Godfrey na kusema kuwa vazi hilo ni kiashiria cha kuwaleta pamoja wafrika.
"Godfrey ni Mbunifu mwenye juhudi hivyo wasanii wanatakiwa kufanya juhudi ndio Dominic"
Amesema kuwa Serikali inamuunga mkono Godfrey kwa jitihada zake "Sisi tunamuunga mkono Dominic ili kuhakikisha Ndoto ya Dominic na Vijana wengine kutimia"
Dominic Godfrey Mbunifu wa mavazi ya Tribe Called Afrika amesema vazi hilo ni ubunifu linaloonyesha uhalisia wa Mtanzania na Mwafrika.
"Nimetengeneza vazi hili kwa mkono kwa ushirikiano wangu na muigizaji kutoka Uengereza Oris .
Amesema kuwa lengo la Vazi hilo ni kuzidi kuitangaza Tanzania kwa kuwa linaonyesha uhalisia wa Watanzania pia ameshirikiana na Msanii Oris Kutembea kwenye maeneo mbalimbali nchini kupiga picha na vazi hilo kuvitangaza vivutio hivyo.
Oris Erhuero Msanii na Mwanamitindo maarufu nchini uengereza alisema kuwa amefika nchi kwa ajili ya kumsapoti Dominic na vazi hilo litaitangaza Tanzania .
Oris alisema akiwa na vazi hilo amevitangaza kivutio vya Tanzania akipiga picha maeneo yenye kuwavutia .
"Nimevutiwa na Tanzania inasehemu nyingi nzuri tumekwenda Ngorongoro, Serengeti , Kilimanjaro na Zanzibar" alisema Oris.
Maria Charles mdau wa mitindo nchini alisema kuwa vazi hilo litakwenda kuiinua Tanzania kwenye daraja la kimataifa.
"Dominic Godfrey amefanya hili akilenga kuitangaza nchi yetu kwenye anga la kimataifa.
Tunaitangaza Tasnia ya Mitindo" alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...