Shirika la Tanzanite Support linatoa msaada kwa makundi ya vijana kwa kuwapatia elimu na ujuzi katika fani mbalimbali.
TSO
tumedhamiria kubadilisha maisha ya vijana na kuwasaidia kufikia malengo
yao na kujitegemea, Kuwashawishi wao binafsi kufanya vyema, kuwa makini
zaidi na nafasi zao katika nyanja zote za maisha na kazi, kwa kuwapatia
taarifa, uwezeshaji, ukuzaji, ujuzi, huku ukitoa nyenzo muhimu na
ushauri.
Lengo
hasa ni kundi la watu ambao wako katika hali na mazingira
yaliyoathiriwa hasa vijana, wanawake na watoto. Kwa vijana juhudi zetu
ni kwa wale walio katika nyumba za kulea watoto na ambao hawawezi tena
kuhudumiwa katika vituo hivi baada ya kufikia umri wa miaka 18. Lengo ni
kuwawezesha kujisimamia wenyewe baada ya kuondoka kwenye vituo vyao.
Tunafanya hivi kupitia elimu na uwezeshaji wa kiuchumi. Tunawaingiza
katika programu yetu ya “Achieving Self-Reliance” (ASR) ambayo
inawatayarisha kutekeleza malengo yao. Tunafanya kazi haswa na vijana
wenye umri wa miaka 15-18 kwa mpango huu.
Tunafanya
kazi na wadau mbalimbali katika hatua zote za programu zetu. Vituo vya
kulea watoto na mashirika mengine ambayo yanaweza kufikia vijana
wanaoishi katika mazingira magumu. Tunawaleta katika kituo chetu na
kuwapatia mafunzo, na kozi za kujiandaa kwa maisha ikijumuisha afya ya
akili.
Katika kila hatua tunafanya kazi na washirika ambao aidha, hutoa huduma kama vile mafunzo ya kujitolea, mpango wa stadi za maisha na matokeo yake ni kuwapatia mafunzo ya kazi na ajira ambayo TSO inafuatilia ili kuhakikisha walengwa wanaishi maisha yenye mafanikio na kutimiza malengo yao.
Tembelea www.https://tanzanitesupport.org
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...