Na Jane Edward, Arusha


Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Arusha wamekutana na wadau wa sekta ya utalii ili kujadili uelewa wa pamoja juu masuala ya kikodi sanjari na kusikiliza changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Hayo yamesemwa jijini Arusha katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii.

Naibu kamishna wa kodi za ndani Swalehe Garugaba amesema kuwa wadau wa sekta ya utalii ni kundi muhimu katika masuala ya Kodi na wapo tayari kuwasikiliza ili kutambua changamoto za kibiashara zinazo wakabili katika suala la ulipaji kodi.

"Sisi tunakusanya kodi lakini wadau muhimu wanao lipa Kodi moja wapo ni sekta ya utalii,na kwa kikao hiki tunaamini kitazaa matunda"Alisema

Ameongeza kuwa kukutana na wadau hao ni katika kuwafanya wafanyabiashara wa sekta ya utalii kufanya shughuli za utalii kwa uharahisi Bara na Visiwani pamoja na kupunguza mlundikikano wa kodi.

Kwa upande wake kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar Yusuph Juma Mwenda amesema wao kama Zanzibar wapo kwaajili ya mashirikiano ya kurahisisha biashara kwa wafanyabiashara kwaajili ya kukuza mapato.

Amesema kuwa Tanzania Zanzibar sekta ya utalii ndiyo inawezesha kukuza uchumi wa Zanzibar kwa zaidi ya asilimia arobaini.

Naye makamo mwenyekiti wa chama cha wakala wa utalii Tanzania (TATO)Henry Kimambo amesema kwa sasa kumekuwa na changamoto za kimfumo ikiwemo kodi ya VAT ya Tanzania Bara ambayo ni asilimia 18 tofauti na Zanzibar ni asilimia 15.

Kennedy Edward ni mtendaji Mkuu wa chama cha wamiliki wa mahotel katika sekta ya utalii Tanzania amebainisha kuwa kukutana kwao na mamlaka ya mapato Tanzania wanaamini wataendelea kuboresha mahusiano yao katika masuala ya kikodi kwa wawekezaji ambao wapo Tanzania kwa sasa na wanaotarajia kuja kuwekeza nchini.

kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar Yusuph Juma Mwenda akizungumzia ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Zanzibar katika kukuza utalii.

Henry Kimambo Makamo mwenyekiti wa chama cha mawakala wa utalii Tanzania TATO akiteta jambo na waandishi wa habari.

Kennedy Edward mtendaji Mkuu wa chama cha wamiliki wa mahotel katika sekta ya utalii Tanzania akizungumzia uwekezaji wa mahotel hapa nchini kwenye utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...