Na Jane Edward, Arusha

Wakulima nchini wametakiwa kuzalisha chakula bora na salama kwa kufuata kanuni bora za kulima kilimo Ikolojia ili kuweza kusaidia walaji kutopata madhara yanayo weza kutokea kutokana na kemikali za viwandani.

Akizungumza wakati wa ziara fupi ya kutembelea eneo la duka ambalo linauzwa vyakula ambavyo vimelimwa kwa kufuata kanuni za kilimo Cha Ikolojia.

Damian Sulumo afisa program mtandao wa wakulima Mviwarusha anasema wanaendelea kufundisha wakulima wa kawaida na wakulima binafsi kwa lengo la kuwasaidia kulima kilimo cha Ikolojia na kuacha kutumia kemikali na mbolea zenye viambata sumu.

 "Tunataka tuondoe kilimo cha mazoea kulima kwa kutumia mbolea nyingi,kemikali nyingi bila kuangalia usalama wa chakula tunacholima pamoja na afya ya Ardhi yenyewe "Alisema Damian

Ayesiga Bubelwa ni Meneja program kutoka IDP anasema kwa kushirikiana na Mviwarusha wameamua kuhamasisha kilimo cha kiikolojia ili kiweze kusaidia jamii kuwa na mfumo wa kula chakula safi na salama.

Aidha anasema  kama mradi wa kilimo endelevu wamekuwa na hamasa ya uanzishwaji wa maeneo ya masoko yatakayo rahisisha upatikanaji wa vyakula vya kiikolojia kwa manufaa ya walaji.

Amesema kilimo hicho kina tija na baadhi ya wakulima wameanza kunufaika kutokana na kilimo Ikolojia ambacho kinaacha ardhi ikiwa salama na chakula kina kuwa bora kwa mlaji.

Hata hivyo mpaka hivi sasa wakulima waliofikiwa moja kwa moja ni  zaidi ya mia nane na elimu ya kilimo Ikolojia kwa kutumia mbegu za asili ambazo zinazo bionwayi ambayo ilikuwa ikilisha walaji kwa wakati wote kabla ya kemikali kufika .

Mradi wa kilimo endelevu ni wa miaka mitano ambapo wameanza mwaka huu lengo ni kuhakikisha wakulima wanaondokana na kilimo cha mazoea huku wakiitaka serikali kupitia wizara ya kilimo kuunga mkono jitihada hizo kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na Cha baadae.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...