WASHITAKIWA wawili wanaotuhumiwa kukutwa na vipande tisa vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 30,000 wameiomba Mahakama isiwasomee maelezo ya kosa licha ya upelelezi katika kesi hiyo kukamilika kwa kuwa wao ni wagonjwa.

Badala yake wameiomba mahakama kuwapeleka katika mahabusu ya keko wakati wakisubiri kupona kwa kuwa gerezani Keko ni pazuri na pasafi sana.

Washtakiwa hao, Hassan Sangari (22) mkazi wa Kingula mkoani Dodoma na Nassoro Mbuguni Mkazi wa Kibasila, Pwani wameomba hayo leo Oktoba 3, 2022 mara baada ya upande wa Jamuhuri kumaliza kuwasomea kesi yao ya kukutwa na nyara za serikali kwa mara ya kwanza.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, Faraja Ngukah mbele ya Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imedai kuwa, Juni 9,2018 eneo la Kimara, Stopover walikutwa na vipande tisa vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 30,000 sawa na sh 66,720,000 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Baada ya kumaliza kusomewa shtaka lao washtakiwa walinyoosha vidole na kuomba Hakimu Shaidi kuwapangia mahabusu ya gereza la Keko, kwa sababu huko ni panzuri, pa safi na pia wameshapata marafiki ambao wanawasaidia kama sabuni na vitu vingine

Pia, washtakiwa hao hawakutaka kusomewa maelezo ya awali kwa madai kwamba wanaumwa, na mmoja alidai kwamba wamekaa gerezani kwa kipindi cha miaka mitatu ana dozi ya kifua hivyo hawezi kuendelea na kesi.

Pia wameiomba Mahakama wapewe viatu vyao vilivyopotea katika Kituo cha Polisi Kati (Central).

Hata hivyo, Hakimu Shaidi aliwaeleza washtakiwa kwamba yeye hausiki na masuala ya kupanga gereza, kwani mtu ambae ana husika na pia kuhusu vitu vyao walivyoviacha kwenye gereza hilo ni kwamba popote watakapokwenda watapelekewa.

Kufuatia hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 18, 2022 kwa ajili ya usikilizwaji wa hoja za awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...