Na Karama Kenyunko
MRATIBU wa Mbio za Ocean City Community Season 2 kati ya Kampuni ya One Plus, Franklin Tissa amesema wanatarajia kutoa bima za afya zaidi ya 200 kwa watoto yatima ambao wanaishi katika vituo vya kulelea watoto.
Tissa amesema hayo leo Oktoba 4, 2022, baada ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuzindua mbio hizo za msimu wa pili ikiwa na lengo la jamii kufanya mazoezi kwa ajili ya kuwa na afya njema.
Amesema hatua hiyo ni kuendelea kuiunga mkono Serikali katika mchakato wake bima kwa wote, ambapo hivi sasa mchakato wa utungaji wa sheria unaendelea na pia lengo lingine ni kuhakikisha jamii inafanya mazoezi.
Pia, Amesema ili kufanikisha hilo wameungana na wadau mbalimbali kwa kuweka kuunganisha nguvu za pamoja ili waweze kutimiza suala la bima na utoaji wa zawadi kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza atapewa gari.
Amesema nguvu hiyo waliyoiunganisha itakuwa na zawadi za kushtukiza ambazo hawataweza kuzitaja kwa sasa hivi kwa hiyo watu wanatakiwa wajitokeze katika mbio hizo ili kukamilisha lengo.
Amesema, mashindano hayo ya Ocean City Community Marathon yatahusisha wakimbiaji na wanariadha na yatafanyika Desemba 31, mwaka 2022 katika Viwanja vya The Green Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Tissa amesema mashindano hayo yatahusisha mbio za umbali wa Km 21.2, Km 10 na Km 5 na zitafanyika tarehe hiyo.
Kwa upande wake, George Obado kutoka Property International amesema wataendele kuwa pamoja na Ocean City Marathon kwa lengo la kuwasaidia watoto, ambapo msimu wa kwanza walitoa zawadi kwa mtoto wa kike na wakiume.
Naye mwakilishi kutoka Chama cha Ridhaa, Mkoa wa Dar es Salaam Rahim Kalyango ameipongeza Ocean kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa na pia wamekuwa wakiwataarifu hatua zote.
Naye baba wa mtoto aliyeshinda mbio hizo Season 1, Robert Chacha alishukuru Ocean na wadau wengine kwa kumpatia mtoto wake, Roman hati ya kiwanja kilichopimwa baada ya kushinda mbio hizo.
"Muwe na moyo huu huu wa kusaidia jamii kwa sababu mnavyofanya hivi mnafanya kazi ya Mungu,"amesema Chacha
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ( watatu kulia) akizindua rasmi mbio za Ocean City Community Season 2 uliyofanyika katika hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam. Wa pili Julia ni ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International Ltd, George Obado.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akiomba dua kwaajili ya kuzindua rasmi mbio za Ocean City Community Season 2 uliyofanyika katika hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa mbio hizo Doris Thomas.
Mwanasheria wa Kampuni ya Property International Ltd, Hazel Chonya ( wa pili kulia) akimkabidhi hati ya kiwanja Robert Chacha mzazi wa mtoto Norman ambae alishinda mbio hizo mwaka jana katika mbio za awamu ya kwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...