Na Mwandishi Wetu,
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Stergomena Tax ameshiriki kwenye Jukwaa la Uchumi kati ya Ureno na Tanzania lililofanyika jijini Lisbon, Ureno.
Kupitia jukwaa hilo, Mhe. Stergomena Tax amewakaribisha wawekezaji kutoka Ureno kuchangamkia fursa za uwekezaji kwenye sekta zenye kipaumbele nchini Tanzania zikiwemo sekta za kilimo, utalii, miundombinu na uchumi wa buluu.
Aidha Waziri Tax ameelezea uwepo wa mazingira mazuri yanayorahisisha shughuli za uwekezaji na kibiashara kwa makampuni yanayokuja kuwekeza nchini Tanzania. Jukwaa hilo liliandaliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ureno wenye makazi yake Paris, Ufaransa, kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya nje ya Ureno na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jukwaa hilo lilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ureno na wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ureno (AICEP).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...