Na Said Mwishehe,Michuzi TV
SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeishauri Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC,) kutekeleza majukumu manne yatakayoleta tija katika sekta hiyo ikiwemo, kuwepo kwa kanuni ya majenzi,sheria yamajenzi,miongozo ya majenzi na kuifanya tasnia hiyo iheshimike.
Akizungumza Dar es Salaam leo Oktoba 20 mwaka wakati wa uzinduzi wa bodi ya baraza hilo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia sekta ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete ameeleza kwamba Serikali inategemea bodi hiyokufanya kazi yake kwa miaka mitatu na kutekeleza majumu waliyopewa.
Amefafanua anazijua changamoto za taasisi hiyo ikiwemo kutopata fedha za maendeleo kwa ajili yakuendeshea shughuli zao za maendeleo, lakini anaamini kuwepo kwa bodi hiyo yenye wataalamu wa kutosha kila kitu kitakwenda sawa ndani ya sekta hiyo.
Ameongeza anaamini bodi hiyo ina uzoefu wa kutosha kwa sababu kila mjumbe ametoka katika taasisi yake hivyo wakijumuika pamoja watafanya mambo mazuri yenye kuleta tija katika taasisi hiyo.
Pamoja na hayo Naibu Waziri Mwakibete ameishauri bodi hiyo kuhakikisha wanaondoa changamoto ya wataalamu wa ujenzi wa barabara kutokuwa na tathimini ya uhakika katika miradi yao.
“Bodi hakikisheni tathimini zinazopelekwa serikalini zinakuwa ni za uhakika na zenye kumaliza mradi uliopo kwani kazi yenu ni kuleta mabadiliko makubwa katika taasisi,'' amesema na kuongeza Baraza hilo lina umuhimu kwa Taifa kwa sababu linachangia asilimia 14 ya pato la Taifa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia sekta ya Ujenzi Ludovick Nduhiye ameongeza kuwa wanategemea mabadiliko mazuri ndani ya taasisi hiyo kutokana na ubora wa bodi iliyopo huki akiitaka bodi hiyo kuhakikisha inatekeleza maagizo waliyopewa ili iweze kuleta tija ndani ya taasisi hiyo na Taifa.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk. Fatma Mohamed ametumia nafasi hiyo kuihakikishia Serikali kuwa bodi hiyo itafanyia kazi kwa weledi yale yote waliyoagizwa ili kubadilisha sura ya taasisi hiyo na Taifa liongeze uchumi.
Dk. Mohamed amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitatu watahakikisha wanafanya yenye kuletatija na mafanikio makubwa kwenye sekta ya ujenzi nchini.Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia sekta ya Uchukuzi Atupele Mwakibete(katikati) akiwa katika picha ya pamo jana wajumbe wa Bodi mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa leo Oktoba 20,2022 baada ya kukutana nakufanya mazungumzo na bodi hiyo.Wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk.Fatma Moamed nawa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa Mhandisi Matiko Mturi.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa Mhandisi Matiko Mturi akifafanua jambo wakari wa kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa bodi mpya ya baraza hilo pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia sekta ya Uchukuzi Atupele Mwakibete pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayesmamia Ujenzi Ludovicky Nduhiye (hawako pichan).
Sehemu ya wajumbe wa bodi mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa wakiwa makini kufuatilia maelekezo na maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia Sekta ya Uchukuzi Atupele Mwakibete(hayuko pichani) wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia Sekta ya Uchukuzi Atupele Mwakibete akiwa makini kusikilia mijada mbalimbali iliyokuwa ikitolewa wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya mpya ya Baraza la Ujenzi la Taifa Dk.Fatma Mohamed(katikati) wakijadiliana jambo na wajumbe wengine baada ya kumalizika kwa kikao chao na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia Sekta ya Uchukuzi Atupele Mwakibete(hayuko pichani)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...