Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Uongozi wa Azam FC upo nchini Afrika Kusini kushiriki mkutano mkubwa wa kujadili soka la Afrika (World Football Summit Africa (WFS) ambao unafanyika siku mbili (Novemba 16-17, 2022) huko Durban.
Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin Popat sanjari na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo, Abdihamid Moallin wapo nchini humo kwa ajili ya mkutano huo.
Viongozi hao wa timu hiyo wamehudhuria mkutano huo huku nyumbani wakiongoza Ligi Kuu Soka Tanzania Bara wakiwa na alama zao 26 katika michezo 12.
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), Almas Kasongo ni miongoni wa washiriki wa mkutano huo mkubwa barani Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...