*wanaoleta wasanii wa Kimataifa Tanzania kuvaana na Basata kisheria*
Na.Khadija Seif,Michuzi TV
BARAZA
la Sanaa Taifa la wakumbusha Taasisi na Makampuni mbalimbali kukata
vibali vya kutumia wasanii kwenye Matamasha mbalimbali yanayofanyika nje
na ndani ya nchi ili kuepuka faini.
Akizungumza
na Wanahabari Novemba 17,2022 Ofisi za Basata Jijini Dar es salaam
Katibu Mtendaji Kedmon Mapana amesema Baraza limeaweka kanuni na
Sheria ili Sanaa ya Tanzania ipewe thamani na isifanyike kiholela bila
kupata kibali kutoka kwa walezi wa Sanaa hiyo ambao ni Basata.
"Imezoeleka
kuwa wasanii wanaingia hapa nchini kufanya kazi za sanaa bila kufata
sheria na kanuni zilizowekwa na kupelekea changamoto mbalimbali
kujitokeza wengine kutotimiza makubaliano ya kufanyika kazi iliyomleta
na tumekua tukiletewa malalamiko mbalimbali ambapo awali sisi kama
Basata hatushirikishwi kwa chochote."
Hata
hivyo Mapana ameweka wazi kuwa Basata imeamua kuwataka Meneja na
mapromota wa wasanii kufika Basata kujisajiri ili kufanya kazi hiyo
kihalali huku akisisitiza zaidi kwa Kampuni na Taasisi watakaofanya
Matamasha bila vibali watatozwa faini au kufungiwa kabisa .
"Kibali
kwa Matamasha ya wazi bila kutozwa kiingilio laki 3 na ukikutwa huna
kibali utapigwa faini ya shilingi milioni 2, kwa Matamasha ambayo
yakutozwa kiingilio anatakiwa kulipa million 2 na akikutwa
hajakamilisha vibali atapigwa faini ya milioni 3 hivyo ili kuepuka
faini hiyo wafike basata kupata vibali vya kuwatumia wasanii kwenye kazi
zao."
Pia amempomgeza
Msanii wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama "Diamond platinum" kwa
kufika Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) pamoja na aliyekuwa Msanii wa lebo
yake "Rayvan" Kumaliza tofauti zao na sasa wanaendelea kufanya kazi kwa
amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...