Na Mwandishi Wetu Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema kuwa, kupitia dhamana ya kuongoza Serikali na nchi, Chama chao kitahakikisha urafiki wa muda mrefu kati ya CCM na Chama cha Kikomunisti cha Cuba (CPC) na uhusiano wa Tanzania na Cuba unaendelea kuimarika zaidi.
Amesema lengo ni kwa ajili ya manufaa na maendeleo ya watu wa pande hizo mbili, kupitia ushirikiano imara kwenye nyanja za kilimo, afya na elimu.
Chongolo ametoa kauli hiyo leo Novemba 2, 2022, wakati alipokuwa akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Yordenis Despaigne Vera, wakati balozi huyo alipofika kumtembelea Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo Jumatano, 02 Novemba, 2022.
Katibu Mkuu Chongolo amefafanua kuwa, Tanzania na Cuba kupitia vyama vya CCM na CPC kwa miaka 60 sasa, zimekuwa na ushirikiano na urafiki wa kihistoria, ulioasisiwa tangu wakati wa viongozi waasisi wa mataifa hayo, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Fidel Castro katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo viongozi wa sasa, kupitia vyama na serikali hizo, wanao wajibu mkubwa wa kuimarisha zaidi na kuuendeleza kwa ajili ya tija na ustawi kwa jamii za nchi hizo.
Kwa upande wake, Balozi Yordenis Despaigne Vera ameeleza kuwa ni muhimu na lazima, kwa pande hizo mbili kuendelea kufanya kufanya kazi kwa pamoja zaidi ili kuendeleza uhusiano na urafiki ulioanzishwa na waasisi hao na kujengewa misingi imara kwa miaka kupitia vyama vya CCM na CPC.





Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Komredi Yordenis Despaigne Vera (kushoto) leo Novemba 2, 2022 katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salaam.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimkabidhi zawadi ya Vitabu Balozi wa Cuba nchini Tanzania Komredi Yordenis Despaigne Vera (kushoto) leo Novemba 2, 2022 mara baada ya kumaliza mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...