Na Mwandishi wetu, Babati
MWENYEKITI
mstaafu wa jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) Mkoa wa Manyara, Johanes
Darabe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa Mkoa huo.
Hata
hivyo, uchaguzi wa nafasi hiyo ilibidi urudiwe kutokana na mshindi
Darabe kutopata zaidi ya nusu ya kura za wajumbe 522 waliohudhuria kati
ya wajumbe halali 616.
Mkuu
wa Wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera, ambaye ndiye amesimamia
uchaguzi huo amesema awali Darabe alipata kura 208 na kuwashinda
wagombea wenzake wawili.
Dk
Serera amesema mbunge mstaafu wa Babati vijiji, Vrajlal Jituson amepata
kura 183 na Mwenyekiti wa wazazi aliyemaliza muda wake Fratern
Kwahhison akapata kura 131.
Dk
Serera amesema uchaguzi huo ukarudiwa kwa mara ya pili kwa wagombea
wawili ambapo Darabe akapata kura 290 na Jituson kura 231.
'Wajumbe
522 walipiga kura za nafasi ya Mwenyekiti kwa mara ya kwanza na raundi
ya pili wakapiga kura wajumbe 521 huku kura mbili zikiharibika," amesema
Dk Serera.
Mkuu huyo wa
wilaya ya Simanjiro, pia amemtangaza Pasian Siay kuwa mjumbe wa baraza
kuu la wazazi Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, baada ya kuwashinda
wapinzani wake Willbroad Bayo na Stephen Manda.
Amemtangaza pia Carol Gisimoy kuwa mjumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa wa Manyara kupitia jumuiya ya wazazi.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt Suleiman Serera (kushoto) ambaye ni msimamizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, aktoa maelekezo wakati akisimamia uchaguzi huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...