Na Mwandishi wetu, Babati
MJUMBE wa Baraza la UWT Mkoa wa Manyara, Mwalimu Digna Nyaki amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Mkoa wa Manyara kwa kumchagua kwa kishindo kuwa Mjumbe wa baraza la UWT wa Mkoa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria Makota ambaye ni msimamizi wa uchaguzi huo amemtangaza Digna Nyaki kuwa ameshinda nafasi hiyo kwenye uchaguzi huo uliofanyika Mjini Babati.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kushinda nafasi hiyo Digna amewashukuru wajumbe wenzake kwa kumpatia kura za ndiyo na kushika nafasi hiyo.
"Nawashukuru wanawake wote ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT Mkoa wa Manyara kwa kunichagua na kuibuka kidedea kushika nafasi hii," amesema Digna.
Ametoa ahadi kwao kuwa atawawakilisha vyema kwenye nafasi yake ya mjumbe wa baraza la UWT Mkoa huo wa Manyara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...