Na Mwandishi Wetu, Same
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo amepongeza Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela kwa kuanzisha Mashindano ya Kilango Cup kwani yanaleta Umoja na mshikamano kwa wananchi
Akizungumza kwenye fainali za Mashindano hayo Mpogolo amesema mbali ya kujenga umoja na mshikamano pia yanasaidia kuibua vipaji vya soka kwa vijana wa Tanzania.
Aidha amesema malengo mengine ya mashindano hayo ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga nchi yetu hasa kwenye kilimo na biashara.
Pia amesema michezo husaiia vijana kuachana na mambo yasiyofaha katika jamii huku akisisitiza kwamba kazi ni msingi mkubwa wa maendeleo
Kwa upande wake Mbunge wa Same Mashariki Anne kilango amesema mashindano haya ni endelevu na lengo ni kuwaweka vijana wawe pamoja na kutengeneza timu ya jimbo ambayo itakayofanya vyema kwenye mashindano makubwa
Pia amesema zaidi ya vijana 1200 wameshiriki mashindano hayo na kusisitiza kuwa mashindano hayo ni juhudi za kumuunga mkono Rais Samiha Suluhu Hassani kwani na yeye ni mmoja wa wadau wanaopenda michezo hapa nchini .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...