Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Chama Cha Mapinduzi( CCM )Mkoani Pwani,kimeanika mkeka wa majina ya wanachama walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali Jumuiya na Chama ,huku kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya Mwenyekiti inagombewa na Shaibu Ally Mtawa ,Farida Mgomi, Mwinshehe Mlao na Imani Madega.
Kaimu Katibu CCM Mkoani Pwani, Elisante Msuya alitaja wagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa MNEC kutoka mkoa ni , Mohammed Mchengerwa, Mbaraka Kitwana Dau, Muhammed Mussa Mtuliakwaku, Alhhudi Shilla na Nunu Daudi Kanza.
Msuya alisema nafasi ya mwenezi mkoa kwasasa nafasi hiyo haipo katika mchakato huo , Utaratibu utatolewa Lakini kwa kipindi hiki wanaotaka nafasi hiyo watateuliwa na kuajiliwa kama watumishi wa mikataba kwa kipindi cha miaka mitano.
Msuya alieleza ,uchaguzi wa CCM mkoa utafanyika Novemba 21 mwaka huu (jumatatu ijayo).
Wakati huo huo Msuya ambae pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoani humo ,alitaja walioteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti ni Josian Kituka, Veronica Kilango na Zainab Amiri Gama.
Nafasi ya mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu Taifa ni Wakati Mtulia ,Rugemalira Rutatina ,Tatu Kano na Hamis Dambaya.
Uwakilishi kutoka Wazazi kwenda UVCCM ni Shabiri Omari Boban ,Said Athuman na Maneno Aziza Bingwa .
Uwakilishi kutoka Wazazi kwenda UWT ni Faith Silla Munanka, Catherine Katele na Helena Veradiana Masanja na uchaguzi utakuwa Novemba 18 mwaka huu.
Katika hatua nyingine,Katibu wa Jumuiya ya Vijana Mkoani Pwani ,Kisamba Said Kidando alieleza , nafasi ya Mwenyekiti Jumuiya hiyo ni wanne ambae ni Omary Maulid Mkongo,Samaha Seif Said ,Adam Salehe na Abuu Omary.
Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa ni Juma Seif , Mohammed Mwinchumu na Mufandii Hamis Msagaa.
Kidando alieleza kwamba , UVCCM kuwakilisha UWT wagombea ni Zainab Karim Ramadhani,Rehema Idris na Maria Protas Msimbe.
Kuwakilisha Wazazi watakaogombea ni pamoja na Ashura Thomas ,Jafari Swai,Swed Iddi Salum na Hassan Said,na uchaguzi wa Jumuiya hii umetajwa kufanyika Novemba 16 mwaka huu.
Vilevile Upande wa Jumuiya ya Wanawake (UWT)Katibu wa UWT Mkoani Pwani,Fatuma Ndee alieleza wagombea nafasi ya Mwenyekiti ni Rehema Ngatanda ,Safihuna Bakari Singo, Joan Tandau na Zainab Vullu.
Baraza Kuu la UWT mkutano mkuu wa CCM Taifa ni Mariam Ibrahim,Dionisia January Malobola, Judith Mluge na Nancy Mutalemwa.
Ndee alifafanua kuwa ,nafasi ya mkutano Mkuu wa CCM mkoa mgombea ni Mary Omary Mseja ,Mary Frolian Nchimbi.
Kuwakilisha UWT katika vikao vya UVCCM mkoa ni Nyamsumi Dingubita ,Christina Anania Enry na Fatuma Ally Ndugu.
Kuwakilisha katika vikao vya Jumuiya ya Wazazi mkoa ni Zainab Gama,Fatuma Juma Mkoga na Mary Mseja,na ameongeza kuwa uchaguzi wa UWT utafanyika Novemba 17 mwaka huu.
Home
HABARI
WANNE KUCHUANA KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI CCM MKOANI PWANI,YUMO MADEGA,MGOMI,MTAWA NA MLAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...