Mwenyekiti wa Chama cha Uhifadhi na Uwindaji Tanzania (TACHA,) Kanali Thomas Ndonde (rtd) akizungumza wakati wa mafunzo hayo na kuiomba Serikali kufungua rasmi shughuli za uwindaji zilizozuiwa kwa miaka mitatu sasa, Leo jijini Dar es Salaam.
WAMILIKI
na Watumiaji wa silaha za moto za kiraia
wanaojihusisha na shughuli za uwindaji kupitia Chama cha Uhifadhi na
Uwindaji (TACHA) wamepewa mafunzo maalum ya kujengewa uwezo, umahiri na
kujiamini zaidi katika matumizi ya silaha hizo, huku ombi kubwa
likitolewa kwa Serikali kuruhusu kuendelea kwa shughuli za uwindaji
zilizofungwa kwa
miaka mitatu mfululizo.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Shabaha leo
jijini Dar es Salaam Mratibu msaidizi wa mafunzo ya umahiri wa utumiaji
na utunzaji wa silaha za moto za kiraia nchini kutoka Shirika la
Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi (TPFCS,) Ravent Vedasto amesema,
mafunzo hayo yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya The Firearms and Ammunition Control
Act ya mwaka 2015.
"Leo
tupo katika viwanja hivi vya shabaha chini ya Jeshi la Wananchi Dar es
Salaam kwa kushirikiana na Chama cha Uhifadhi na Uwindaji (TACHA,)
ambao ni wamiliki na watumiaji wa silaha maalum kwa shughuli za
uwindaji...Tunafanya hivi ili kuwajengea uwezo wa kuzitumia na kubaini
wale wanaozitumia kimakosa na kuwajengea kujiamini zaidi ili waweze
kuzitumia vizuri zaidi." Amesema.
Aidha
amesema, kwa miezi mitatu kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu jumla ya
raia 1200 kupitia mwavuli wa TACHA wamesajiliwa na kupatiwa mafunzo na
Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi Tanzania ( TPFCS.) ambalo
pia
linahusika na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi, umahiri
wa matumizi na utunzaji wa silaha pamoja na ulinzi binafsi.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo
pia yanakwenda sambamba na maandalizi na msimu wa Uwindaji ikiwa
Serikali itaridhia na kuruhusu Uwindaji na Uhifadhi baada ya kutoruhusu
zoezi hilo kwa miaka mitatu mfululizo.
"Serikali
yetu ni sikivu na elewa tunaamini itafungua tena anga la uwindaji na
sisi kama wahusika tuna uelewa kupitia mafunzo mbalimbali ya namna hii
yanayotolewa na tupo tayari kwa uwindaji kwa kufuata sheria na matakwa
ya Serikali."
Vilevile
ametoa wito kwa Wizara ya Utalii na Maliasili kutoa kibali kwa wawindaji
kwa msimu ujao wa uwindaji ambao kwa kiasi kikubwa huchangia kukua kwa
uchumi wa Nchi, uhifadhi wa rasilimali za utalii pamoja na kuchangia kwa
kiasi kikubwa katika utoaji wa ajira.
Chama
cha Uhifadhi na Uwindaji Tanzania ( TACHA,) kina jukumu la kuwinda na
kuhifadhi rasilimali za utalii kwa kuzingatia kanuni na miongozo
iliyowekwa na Serikali na ombi lao kubwa kwa sasa ni kwa Serikali
kufungua anga la uwindaji lililofungwa kwa miaka mitatu mfululizo.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yameanza kwa nadharia mapema leo na yatahitimishwa
kwa vitendo ili kuwapika vilivyo wamiliki hao juu ya umiliki na matumizi ya silaha na yamedhaminiwa na kampuni ya Orexy Gas kupitia kampeni ya kutumia nishati ya gesi na kutunza mazingira.
Insp. wa Polisi Vincent Buluba kutoka TPFCS akitoa mada katika mafunzo hayo.
ASP
Hamis Luyeko akitoa mada katika mafunzo hayo ya umiliki wa silaha kwa
wanachama wa Uhifadhi na Uwindaji (TACHA,) yaliyolenga kuwajengea
umahiri zaidi katika kuzitumia, Leo jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...