Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu maswali ya Waandishi wa Habari pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini China na Misri kwenye Mkutano uliofanyika leo Novemba 12, 2020 Ikulu Jijini Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema katika Mkutano 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27), Tanzania imekuwa ni nchi kinara katika uandaaji wa Mwongozo wa Biashara ya Hewa ya Ukaa.

Amesema hayo leo Novemba 12, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bi. Zuhura Yunus na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini China na Misri hivi karibuni.

Dkt. Jafo alisema hapo hapo mwanzo hatukuwa na kanuni wala mwongozo wa biashara hii na hivi sasa kukamilika kwake kutasaidia Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari alisema katika mkutano huo unaendelea Sharm El Sheikh nchini Misri alimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyeungana na wakuu wengine wa nchi zinazoendelea kupaza sauti kuzitaka nchi zinazoendelea kutimiza wajibu wao.

“Ni kweli changamoto ya uzalishaji wa hewa ukaa ni kubwa na nchi yoyote dunia inapofanya uchafuzi huo wa hewa zinaathrika nchi zote duniani na ndio maana wataalamu wanatuambia ifikapo mwaka 2050 kuna uwezekano barafa katika mabara mbalimbali katika milima ukiwemo Kilimanjaro zitayeyuka kutokana na ongezeko la joto,” alisema.

Waziri Jafo alisema kutokana na hali hiyo Mkutano wa Paris wa mwaka 1992 uliazimia nchi zinazoendelea ambao ndio wazalishaji wakubwa wa hewa ukaa wanapaswa kuchangia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 100 kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

‘Kutokana na msukumo mkubwa kwa nchi zinazoendelea kutakiwa kutoa fedha, tayari katika awamu iliyopita Tanzania ilipokea Dola za Marekani milioni 23.6 na kwa mgao unaotarajiwa kutolewa tutapata Dola za Marekani milioni 52.8 na hii ni ni kutokana na efforts (jitihada) zilizofanyika katika Mkutano uliopita wa COP26,” alisema.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...