TAASISI ya Doris Mollel ambayo inahusika na kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Watoto Njiti), Novemba 15, 2022 ilizindua maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo kwa kawaida huadhimishwa ifikapo Novemba 17  ya kila mwaka.
 
Ila kwa mwaka huu Taasisi hiyo imepanga kufanya maadhimisho hayo kwa namna ya kipekee na kilele chake kitakuwa tarehe 20 Novemba 2022 katika viwanja vya Robanda, vilivyopo wilayani ya Serengeti, mkoani Mara.  
 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel,  Doris Mollel alisema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yaanzia kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambapo wadau mbalimbali watashiriki zoezi la kupanda parachuti zenye jumbe mbalimbali kuhusu Mtoto Njiti na baadaye kwenye kilele katika viwanja vya Robanda, vilivyopo wilayani ya Serengeti, mkoani Mara.  
Katika maadhimisho hayo, Taasisi ya Doris Mollel itakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 180, ambavyo vitakwenda katika hospitali za wilaya za Serengeti, Ukerewe, Kwimba, na Magu.
 
Aliongeza kuwa pamoja na kukabidhi vifaa hivyo, pia kutakuwa na zoezi la ufungaji wa mitambo ya hewa (Oxygen Machine)  kwenye wadi za watoto wachanga katika hospitali za Siha, Karatu, Monduli na Dabaldi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 47, pia itakabidhi mitungi 200 ya gesi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 8, kwa ajili ya wadi ya wakina mama wajawazito katika hospitali ya Wilaya ya Serengeti.
 
Katika siku hiyo, Taasisi ya Doris Mollel, wamepanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini, ambao ni; TIKA, Aga Khan Hospital, Oryx Energies Tanzania, Freo2 Foundation, Miracle Experience, Coca Cola Tanzania, Precision Air Tanzania, Anudha Limited, Ashton Media, Nest360, na Ifakara Health Institute, ambao kimsingi, wamefanikisha kwa kiwango kikubwa maadhimisho hayo kuhakikisha Siku ya Mtoto Njiti inafana.  
 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...