Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Uswizi, Breel Embolo alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 48 katika mchezo wa Kundi G dhidi ya timu ya taifa Cameroon katika dimba la Al Janoub nchini Qatar.

Mshambuliaji huyo hakushangilia bao hilo kutokana na asili yake ni Cameroon kwa Kuzaliwa, baada ya Wazazi wake kutengana akiwa na miaka mitano, Mama yake alihamia nchini Ufaransa kwa masomo kwa kile kilichoelezwa.

Mama yake Mzazi Embolo, akiwa nchini Ufaransa alikutana na Mwanaume mmoja raia wa Uswizi, mwaka 2014, Mshambuliaji huyo alibadili uraia na kuwa raia wa nchi hiyo na kwa mara ya kwanza alicheza Ligi Kuu Soka nchini Uswizi katika Klabu ya FC Basel.

Embolo, akiwa na umri wa miaka 25 alisajiliwa na Klabu ya Schalke 04 mwaka 2016, baadae alienda kucheza kucheza Borussia Monchengladbach mwaka 2019 kwa mkataba wa miaka minne.

Kwa sasa anacheza Klabu ya Monaco ya Ufaransa na amefunga mabao 8 katika michezo 23, katika mashindano yote, katika Michuano ya Kombe la Dunia anaiwakilisha Uswizi wakiwa Kundi moja na timu za Brazil, Cameroon na Serbia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...