Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Mlango wa Ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyopata ajali Novemba 6 mwaka huu ulifunguliwa na Muhudumu wa Ndege hiyo na msaada wa Abiria waliokuwa kwenye Ndege.

Prof. Mbarawa amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa ripoti ya awali ya Uchunguzi wa ajali ya Ndege hiyo iliyotokea Mita chache kabla ya kutua katika uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera.

“Ni kweli kuwa Mlango wa Ndege iliyopata ajali ulifunguliwa na Muhudumu wa Ndege, na msaada wa Abiria wa Ndege hiyo, Wananchi waliokuwa wanafanya shughuli za uvuvi jirani na eneo hilo walifika kwenye tukio dakika tano tu baada ya ajali”, amesema Prof. Mbarawa

Prof. Mbarawa amesema zoezi la uokozi baada ya kutokea majanga, linafuata taratibu na miongozo ya mikataba ya Kimataifa katika uendeshaji wake, huku akibainisha kuwa Tanzania inaongozwa na mkataba wa Kimataifa wa Uokoaji wa mwaka 1974 ambao umeridhia watu wa karibu na eneo la ajali kusaidia uokoaji wakati janga linapotokea.

Amethibitisha, kuwa Boti ya Uokozi katika eneo la Ziwa Victoria ambayo inahudumia eneo kubwa katika Ziwa hilo, ilikuwa mbali na eneo la tukio wakati ajali hiyo inatokea siku hiyo ya Novemba 6, 2022, hivyo ilifika katika eneo hilo na kukuta shughuli za uokoji zikiendelea zikihusisha Vyombo mbalimbali na Wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...