Na Said Mwishehe, Michuzi TV

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam imewaomba wakazi wa Mtaa wa Mikenge pamoja na wawekezaji wa maeneo hayo kuwa na subira wakati ufumbuzi wa mgogoro uliosababishwa na kuzibwa kwa barabara ya Mtaa huo unaodaiwa kuzibwa a mwekezaji wa Kampuni ya ASM(T) LTD.

Mgorogoro huo ambao unazaidi ya miaka sasa na hivyo kumsababisha wananchi wa Mikenge kutoa malalamiko yao kutokana na kufungwa kwa barabara ambayo ilikuwa inapita kwenye kiwanja cha Muwekezaji huyo kwenda katika maeneo mengine ya ufukwe wa Bahari ya Hindi ambapo mbali ya kutumiwa na wananchi mbalimbali pia kuna wawekezaji wengine waliokuwa wakiitumia barabara hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Erasto Kiwale amewaambia waandishi wa habari jana kwamba ni kweli wanafahamu kuhusu mgogoro huo na tayari wameanza kutafuta ufumbuzi wake kwa kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria,kanuni na taratibu kwa lengo la kushughulikia jambo hilo kwa kufuata maelekezo yote muhimu.

"Baada ya maelekezo kutolewa na Mamlaka zinazohusika na utatuzi wa mgogoro huo pamoja na vikao ambavyo vimekaa kujadiliana tayari kwa sasa halmashauri imeanza kutekeleza maelekezo yote ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa."Halmashauri tunatambua umuhimu wa wananchi kuwa na barabara lakini pia tunathamini juhudi za wawekezaji wote,hivyo tutatafuta ufumbuzi kwa njia inayostahili ikiwa pamoja na kufuata maelekezo ambayo yametolewa.

"Moja hatua ambazo tunazichukua ni ulipaji na tathimini ya awali ilifanyika na sasa halmashauri na sisi tunaendelea na tathimini ya pili ambayo tunaamini itatoa muelekeo mzuri wa kama kulipa fidia ili ukuta ambao umezuia barabara ya eneo hili ubomolewe.Lakini kabla ya kufika huko lazima tathimini ya kina ifanyike,"amesema.

Aidha amesema kwa kuwa tayari wameanza kushughulikia jambo hilo ni ngumu kueleza kila ambacho kinafanyika kutokana na taratibu zilizopo lakini jambo ambalo wananchi wanatakiwa kufahamu mgogoro huo unashughuliwa na ufumbuzi utapatikana.

"Tunawaomba wananchi pamoja na wawekezaji wote kuwa na subira, mgogoro tunaushughulikia na maelekezo ambayo tunayo tumeanza kufanyia kazi.Ni jambo ambalo linahitaji kufuatwa kwa taratibu zote,hivyo wakati tunashughulikia tunaomba subira iwepo kwa pande zote,"amesema na kukiri mgogoro huo ni wa muda mrefu lakini ni vema ikaeleweka ulipaji fidia ni mchakato na una mchakato wake ambao lazima ufuatwe.

Aidha amesema matarajio yao ni kuona wananchi wa maeneo hayo wanakuwa na barabara ya kupita lakini wakati huo huo wawekezaji ambao wako eneo hilo nao wanafanya shughuli za uwekezaji katika mazingira mazuri."Wakati tunaendelea kutatua mgogoro kuna barabara ambayo Halmashauri iliitengeneza kwa muda lakini wananchi wanalalamika umbali ukilinganisha na barabara ya awali waliyokuwa wakiitumia kabla ya kuzibwa na ukuta."

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikenge Lameck Mayala pamoja na mambo mengine ni vema Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali Kuu wakaumaliza mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu na kwa kiasi kikubwa unachangia Kurudisha nyuma shughuli za kiuchumi kutokana na kuzibwa kwa barabara ya eneo hilo

Ameongeza kwamba barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa watu wengi wanaokwenda baharini kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za uvivu na wengine kwenda maeneo yenye uwekezaji ,hivyo wanaiomba Serikali kutafuta suluhu ili ukuta ulioziba barabara hiyo ubomolewe.

Amefafanua kuzibwa kwa barabara hiyo kumesababisha hata Hoteli nyingine ambazo uwekezaji wake umetumia fedha nyingi zimefungwa kwasababu magari yanashindwa kufika kwasababu tu ya ukuta ambao umejengwa. "Kuna watu walikuwa wakifanya kazi kwenye hoteli hizo lakini hivi tunavyozungumza hawana kazi."

Akizungumza kwa niaba ya wawekezaji wengine wa maeneo hayo ambao wanalalamika kufungwa kwa barabara hiyo Vidate Msoka ameeleza wao hawana tatizo na Muwekezaji huyo bali wanachotamani kuona barabara iliyokuwepo awali inapatikana na shughuli za uwekezaji wanazofanya ziendelee kwa maslahi ya pande zote.

"Tunaiomba Wilaya yetu ya Kigamboni kumaliza mgogoro huu kwa kuharakisha utatuzi wake.Ikifunguliwa na sisi pamoja na watumiaji wengine wa barabara hii tutaendelea na shughuli zetu ambazo kwa sasa zimesimama."

Wakati huo huo Mwekezaji mwingine wa eneo hilo Arif Sheikh, ametoa pongezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni kwa hatua ambazo imeanza kuchukua kushughulikia mgogoro huo lakini ombi lake ni kwamba ufumbuzi uharakishwe ili waendelee na shughuli zao.

Amesema katika kushughulikia mgogoro huo wameshakaa vikao vingi na umefikia Waziri wa Nyumba na Maendeeo ya Makazi Dk.Angelina Mabula."Tunachofahamu Kuna fidia inatakiwa Kulipwa ili barabara hiyo ipatikane.Ombi letu ulipaji fidia ufanyike haraka."

Kwa upande Juma Shaban Mkazi wa Mikenge amesema wamekuwa na changamoto ya kufika kwenye shughuli zao tangu kuzibwa kwa barabara ambayo imekuwepo kwa miaka mingi."Tunaomba jambo hili lifike mwisho,tumelalamika muda mrefu."


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...