Na Fredy Mgunda, Iringa.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imeyaipongeza makampuni ya Asas kwa kupata tuzo ya ulipaji Kodi bora kutoka kwa mamlaka ya mapato(TRA) jambo linalosaidia kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada alisema kuwa Halmashauri makampuni ya Asas yamekuwa yanalipa Kodi vizuri na kuchangia maendeleo ya wananchi wa Halmashauri hiyo.
Ngwada alisema kuwa makampuni hayo yamekuwa yanalipa kodi kwa wakati bila kufanya ujanja ujanja wowote ule kwa mamlaka husika.
Alisema kuwa kulipa Kodi kwa makampuni hayo kunasaidia kulipa mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali na kuchangia shughuli za kimaendeleo ambazo zitachangia kukuza uchumi wa Taifa.
Meya Ngwada alisema kuwa wafanyabiashara Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa wanalipa bilioni moja na laki nane lakini Kati ya Kodi hiyo makampuni ya Asas yamekuwa yanalipa Kodi Kati ya Milioni mia nane hadi Milioni mia tisa.
"Katika kufanya kazi za kimaendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inategemea walipa Kodi kufanya shughuli za kimaendeleo na kukuza uchumi wa Halmashauri hiyo" alisema Ngwada.
Alisema kuwa wanaipongeza makampuni ya Asas kwa kuwa na mchango mkubwa wa kimaendeleo katika Manispaa ya Iringa Kwa kujenga majengo mbalimbali kama ofisi za meya wa Manispaa ya Iringa,jengo la ustawi wa jamii,ofisi za ardhi,jengo la watoto njiti,jengo la kuhifadhi damu salama,jengo la viongo bandia na misaada mingi kwa wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Ngwada alimazia kwa kusema kuwa Wananchi na wafanyakazi wa Manispaa ya Iringa wanaendelea kuyapongoze Makampuni ya Asas kwa kupata tuzo ya ulipaji bora wa Kodi jambo ambalo linaleta sura nzuri kwa jamii.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akimkabidhi tuzo ya ulipaji Kodi bora mkurugenzi wa makampuni ya Asas Ahmed Abri Asas
Meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akizungumza na
waandishi wa habari juu tuzo waliyopewa kampuni ya Asas kwa ulipaji bora
wa Kodi kutoka TRA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...