Na Mwandishi Wetu
Timu ya taifa ya Tunisia imepoteza mchezo wake wa mzunguko wa pili wa Kundi D baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya taifa ya Australia katika mchezo wa Michuano ya Kombe la Dunia uliopigwa kwenye dimba la Al Janoub nchini Qatar.
Katika mchezo huo bao la Australia lilifungwa na Mitchell Duke kwenye dakika ya 23 ya mchezo huo, Wawakilishi wa bara la Afrika, Tunisia wamepoteza mchezo huo huku walifanikiwa kupata sare ya 0-0 dhidi ya Denmark huku Australia wakipoteza mabao 4-1 mbele ya Ufaransa.
Hali ni tete kwa Tunisia baada ya kuwa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Kundi hilo wakiwa na alama moja pekee katika michezo miwili, huku Ufaransa wakiongoza msimamo wakiwa na alama tatu katika mzunguko mmoja.
Australia wakiwa na mizunguko miwili na nafasi ya tatu katika msimamo, wana alama tatu wakati Denmark wana alama moja wakiwa na mzunguko mmoja pekee, mchezo wa mzunguko wa tatu Tunisia atacheza na Ufaransa mchezo uliotajwa kuwa mgumu kwa Wawakilishi hao wa bara la Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...