Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ameelekeza halmashauri zote mkoani humo kuandaa maadhimisho ya wiki ya utoaji elimu ya lishe bora katika ngazi za vijiji ili kukabiliana na tatizo la udumavu.

Ametoa kauli hiyo leo (Novemba 04, 2022) mjini Sumbawanga wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki Kumi na Mbili (12) kwa maafisa lishe wa halmashauri zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la udumavu ambao kwa Rukwa upo asilimia 47.9 kwa takwimu za mwaka 2018.

Sendiga alibainisha kuwa maadhimisho hayo yakifanyika itakuwa jukwaa zuri la wataalam wa lishe kutoa elimu ya uandaaji vyakula bora na ulaji sahihi kwa kutumia vyakula vinavyopatikana kwenye mazingira ya Rukwa kwa kuwa mkoa huo ni mzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula.

Akitoa taarifa ya vifaa hivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Ibrahim Isaack alisema jumla ya pikipiki Kumi na Mbili zimetolewa kwa Halmashauri za Kalambo (4), Sumbawanga Vijijini (3), Nkasi (3) na Manispaa ya Sumbawanga (2).

Dkt. Ibrahim alisema pikipiki hizo zitakwenda kufanya kazi ya elimu ya lishe, kuboresha utoaji chanjo na kufuatilia magonjwa ya milipuko vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kuhusu pikipiki (12) zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maafisa Lishe kwenye halmashauri za Rukwa leo mjini Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki (12) kwa maafisa lishe wa halmashauri za Rukwa zitakatumika kutoa elimu ya kudhibiti udumavu vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kaiwasha moja kati ya pikipiki (12) alizozikabidhi leo kwa Maafisa Lishe wa Halmashauri za mkoa huo ili zikatumike kutoa elimu ya lishe bora na chanjo vijijini. Kushoto ni Afisa Lishe wa Manispaa ya Sumbawanga Bw. Nassoro Chacharika aliyekabidhiwa pikipiki hiyo leo. (Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...