Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Nyangasa akipanda miti aina ya Mizambarau na Midodoma katika eneo la kisima namba 11 kilichopo Kigamboni ambacho ni sehemu ya visima 7 vilivyochimbwa na DAWASA kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa Kigamboni na katikati ya jiji la DSM.
Zoezi la upandaji miti ni moja ya maagizo ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alilotoa alipotembelea mradi wa maji wa Kigamboni kwa lengo la kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...