Na Farida Mangube Morogoro

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Haemed Abdulla ameushauri umoja wa wahitimu wa Chuo kikuu Mzumbe kuanzisha mfuko wa ufadhili (Alumni Scholarship scheme) utakao wasaidia watanzania ambao hawana uwezo wa kifedha na wanasifa za kusoma katika ngazi ya Chuo kikuu.

Mfuko huo utawasaidia wanafunzi wanaoingia chuoni na kuishindwa kuendelea na masomo yao kutokana na ukosefu fedha hivyo kuadhishwa kwake utasadifu kauli mbiu ya umoja huo inasema Tujifunze kwa maendeleo ya watu.

Akizungumza mkoani Morogoro kwenye mkutano wa Baraza la Masajili la chuo kikuu cha Mzumbe Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Heamed Abdulla pia amewataka wahitimu kuongeza juhudi katika kufanya tafiti kwani maendeleo ya nchi yeyote kiuchumi na kiteknolojia hutokana na tafiti na ushauri makini wa wataalamu.

Aidha amekitaka Chuo kikuu cha Mzumbe kuona namna ya kuadhisha ushirikiano na vyuo vya Zanzibar ili kutanua wigo wa kuchagua program za kujifunza na kusogeza fursa ya elimu kwa Wanzanzibar.

Mkutano huo umepisha katiba ya wahitimu ( Walumni Constitution) na mkakati wa kuwashirikisha wahitimu ( Alumni Engagement Strategy ) hivyo ameupongeza uongozi wa Baraza la Masajili chini ya Rais wake CPA Ludovik Utouh kwa kuandaa nyaraka hizo kwani kupishwa kwa nyaraka hizo kutasaidia kuaona namna ya kukisaidia chuo kikuucha Mzumbe.

“Nakipongeza sana chuo pamoja na uongozi wa baraza la Masajili chini ya rais wetu CPA Ludovik Utouh kwa jitihada za kuaanda za nyaraka hizi. Kimsingi nyaraka hizi zitasaidia kuona namna yya kushiriki katika kukiletea maendeleo chuo chetu”.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni mwanafunzi aliyewahi kusoma Mzumbe Christina Mndeme amesema kuwa chuo kikuu Mzumbe kimetoa viongozi wengi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na wataalamu wengine.

Hivyo amewataka wanafunzi wanaosoma chuoni hapo kujivunia na kuona wenye bahati na kwamba baada ya kuhitimu wanapaswa kurudisha fadhira kwa chuo hicho.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amekishauri chuo kikuu cha Mzumbe kuadhisha mafunzo ya mtandao( online study) ili kupanua wigo ukubwa wa kupata wanafunzi na kuongeza mapato ya Chuo pamoja na kukitangaza.

Amewapongeza wahitimu wa Mzumbe kwa kuunda umoja huo na kuwataka kuendelea kuulinda ili kuisaidia Serikali kutimza malengo yake kupitia wasomi hao ambao wameungana na kupia munganiko huo utasida kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi.

Pia amewataka wanzania kudumisha uzalendo kwa nchi yao kwani kila taifa lenye kutaka kukua kiunchumi lazima swala uzalendo lipewe kipao mbele.

Awali Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Mzumbe Profesa Wiliam Mwegoha amesema kuwa kwa sasa chuo kipo kwenye upanuzi wa majengo yake katika eneo la maekani ambapo umejengwa ukumbi, jengo la utawala na ukumbi kwa
ajili ya mahafali.

 










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...