Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya Miaka 50 ya NBAA CPA Dr Neema Kiure kuhusu historia ya Bodi hiyo wakati kufungua maonyesho yenye lengo la kuwaelimisha Wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla jinsi ya kuandaa taarifa za hesabu za Fedha, Kodi na kuwasaidia kwenye nyanja mbalimbali zinazohusu Uhasibu na ukaguzi yanayafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akipatiwa maelezo na Afisa Mwasiliano kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Sheila Mfunami kuhusu namna wanavyosajili makampuni wakati wa ufunguzi wa maonyesho yaliyoandaliwa na Bodi ya NBAA yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akipata maelezo kutoka kwa Meneja Biashara kutoka UBX Rhobi Mwita alipotembelea Banda hilo wakati wa uzinduzi wa maonyesho yenye lengo la kuwaelimisha Wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla jinsi ya kuandaa taarifa za hesabu za Fedha, Kodi na kuwasaidia kwenye nyanja mbalimbali zinazohusu Uhasibu na ukaguzi yanayafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akimsikiliza Mkaguzi wa Ushirika Mkoa ofisi ya Dar es Salaam, Brighton Mwang'onda alipotembelea Banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wadau wa NBAA yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...