Na Seif Mangwangi, Arusha

WANAWAKE na Wasichana zaidi ya 7000 kutoka katika wilaya 7 nchini ambao wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali wanatarajiwa kunufaika na mradi wa ubia wa uwezeshaji kupitia ujuzi(ESP) .

Mradi huo utakaodumu kwa miaka7 na unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania unaelezwa kugharimu Bilioni 45 hadi utakapokamilika ambao wasichana na wanawake hao watapewa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ikiwemo ufundi.

Akifungua mkutano wa majadiliano jana Jijini hapa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Francis Maiko amewataka wasichana na wanawake kujitokeza ili kupata fursa hiyo.

Amesema mradi huo ambapo walengwa watapelekwa katika vyuo vya maendeleo ya wananchi kujifunza ujuzi tofauti utawakwamua kiuchumi na kuwafanya kuondokana na tatizo la ajira.

"Vyuo vya maendeleo ya wananchi vimekuwa taasisi za misingi za kudahili wanafunzi na makundi ya watu waliopo pembezoni ambao wamekuwa wakiacha masomo kutokana na sababu mbalimbali za kimazingira, tutavitumia kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanatimia," amesema.

Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya jinsia ambaye pia ni mshauri wa mradi huo, Dkt. Alice Mumbi amesema mradi huo utawasaidia watoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuwagawia vifaa.

Amesema mradi huo utatekelezwa katika halmashauri 7 za Monduli Mkoani Arusha, Morogoro, Kilwa Mkoani Pwani, Singida, Nzega Mkoani Tabora, Kasulu katika Mkoa wa Kigoma, Tarime Mkoani Mara, Kondoa Mkoani Dodoma na Njombe katika Mkoa wa Njombe.

"Siku ya leo tumekutana hapa jijini Arusha, tunalenga kuwainua watoto wa kike na tunarajia matokeo ya mwisho ya ESP ni kuboresha ushiriki wa wanawake na wasichana kiuchumi nchini Tanzania"ameongeza

Amesema ndani ya mradi huo pia jumla ya wanafunzi 3200 wataweza kushiriki katika shughuli za usawa wa kijinsia na uhamasishaji wa haki za binadamu, huku jumla ya wafanyakazi 180 wataweza kufunzwa ujuzi wa kiufundi na ufundishwaji na kutoa moduli za usawa wa kijinsia na haki za binadamu.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...