Na Ashrack Miraji, Same

NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) DK.Festo Dugange pamoja nabunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Milango Malecela wamekagua kituo cha Afya Kata ya Vunta ambapo wameonesha kutoridhishwa na hadhi ya kituo hicho, kuchakaa kwa majengo na huduma hafifu zinazotolewa.

Akiwa kwenye ziara jimbo la Same Mashariki amesema Dk. Dugange amesema Serikali imetoa Sh.300,000 kwa ujenzi wa awali wa Kituo kipya cha Afya kata ya Vunta ili wananchi wa Kata hiyo na

Amesema ujenzi huo uwanze mara moja kujenga kituo hicho na kuambatana na majengo ya upasuaji na chumba cha kuifadhia Maiti hili wananchi wasipate tabu kutembea zaidi ya kilometa 25 kufata huduma ya afya

Aidha amemshukuri Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela kwa juhudi kubwa anazofanya kuwapambania wananchi wa jimbo lake akiwa bungeni.

"Nimevutiwa na miradi mikubwa ya jimbo hilo ikiendelea vizuri ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Mihamba na zahati kubwa na ya kisasa ambayo imegharimu Sh.500 ujenzi wake ukikaribia kukamilika. Pia na barabara za Tarura ambazo zinajegwa hili kuleta unafuu kwa wakazi wa vijiji vya Same Mashariki,"

Pia amewaomba wanachi wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi anaowaongiza wakiwemo wa Jimbo hilo.

Kwa upande wake Anne kilango ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kumpatia Sh.milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Vunta ambacho amekuwa akikisemea bungeni zaidi ya mara tatu na utekelezaji wake unakwenda vizuri.

Pia ameendelea kueleza kwamba lengo lake ni kuona wananchi wake hawapati tabu kwenye mahitaji muhimu kama afya,elimu, maji, na barabara ili wapitishe mazao yao kwa wepesi zaidi na kuwapatia wananchi miradi tofauti wajikwamue kiuchumi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...