Baadhi ya Picha za washiriki wa kongamano la pili la Afya la Sayansi Shirikishi kuhusu Vimelea Sugu vya Magonjwa dhidi ya Dawa lililofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi washiriki wakipata maelezo kuhusiana na Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya kwenye kongamano la pili la Afya la Sayansi Shirikishi kuhusu Vimelea Sugu vya Magonjwa dhidi ya Dawa lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda MichuzI TV
SERIKALI
imetoa tahadhari kuhusu matumizi mabaya ya dawa za antibiotiki ambapo
imesema kuwa matumzi holela ya dawa hizo husababisha usugu wa vimelea
dhidi ya dawa hali inayoweza kusababisha kupoteza Maisha ya watu na
wanyama.
Kauli hiyo
imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu kwa niaba ya
Waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu wakati akifungua Kongamano la pili la
Afya ya Sayansi Shirikishi kuhusu usugu wa vimelea dhidi ya dawa
iliyofanyika Dar es Salaam.
Prof
Nagu amesema takwimu za tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya dawa za
antibiotiki nchini ni asilimia 92 sambamba na usugu wa asilimia 59.8
ambapo makadirio yanatazamiwa kuwa makubwa katika sekta ya uvivu na
mifugo kutokana na utafiti kuonesha asilimia 90 hutumia dawa za
antibitiki kutibu wanyama badala ya chanjo.
“Leo
tuna matukio matatu kwanza ni kutambulisha mpango kazi wa taifa wa
kupambana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa, pili ni maadhimisho ya wiki
ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa na tatu ni kupokea taarifa ya
utekelezaji wa mpango kazi wa taifa juu ya mapambano ya usugu wa vimelea
dhidi ya dawa (2017/2022).
Amesema
Tanzania kama zilivyo nchi nyingine Duniani kwa kiasi kikubwa
inakabiliwa na janga la usugu wa vimelea dhidi ya dawa katika mapambano
serikali inatekeleza mkakati wa 68 wa kidunia wa mkutano wa afya
duniani wa 2025 .
Amesma
Wizara za Afya, Mifugo na Uvuvi, na Kilimo kupitia Kamati ya Kitaifa ya
Kuratibu shughuri za Kuzuia Usugu wa vimelea Dhidi ya Dawa kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali zimeweka mikakati mbalimbali ili
kukabiliana na changamoto zinazotakana na usigu wa vimelea dhidi ya
dawa.
Wadau wa maswala ya
afya waliokuwepo katika kongamano hilo ni Mradi wa HPSS Tuimarishe
Afya, vyuo vikuu na taasisi za utafiti ambao ndi wamefanikisha
kongamano.
Amesema
Kongamano hili linafanyika katika Wiki ya Kimataifa ya Mapambano dhidi
ya Usugu wa Dawa, ambayo hufanyika kote duniani kuanzia tarehe 18
Novemba hadi tarehe 24 Novemba kila mwaka.
Dk Karin
Wiedenmayer, Mtaalamu Mwandamizi wa Afya ya Umma na Dawa katika Mradi
wa HPSS amesema kongamano la kwanza kuhusu usugu wa dawa nchini
liliandaliwa na mradi wa HPSS Tuimarishe Afya mnamo mwaka 2017 na likawa
na mafanikio makubwa.
“Baada ya miaka mitano tangu
tuandae kongamano la kwanza tunafurahi kuona kwamba wazo letu sasa
limechukuliwa kikamilifu na serikali.''
Dk.
Wiedenmayer piaa alipongeza Serikali na wadau kwa jitihada zao kubwa za
kushughulikia na kupunguza madhara ya usugu wa dawa nchiniTanzania.
HPSS
Tuimarishe Afya ni mradi wa Ushirikiano kati ya Serikali za Uswizi na
Tanzania, unaofadhiliwa na Serikali ya Uswizi na kutekelezwa na Taasisi
ya Uswisi ya Tropical and Public Health Institute
Dk.Karin
amesema Usugu wa dawa ni mojawapo wa matishio makubwa ya afya ya umma
duniani ambayo huperekea kuwa vigumu kutibu maambukizi ya magonjwa ya
kawaida na hivyo kuongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa hayo na vifo.
Dk Karin Wiedenmayer, Mtaalamu Mwandamizi wa Afya ya Umma na Dawa katika Mradi wa HPSS.
Mtaalamu Mwandamizi wa Afya ya Umma na Dawa katika Mradi wa HPSS Dk
Karin Wiedenmayer akitoa maelezo kuhusiana na Mradi wa HPSS
inavyoshiriki katika mapambano ya vimelea sugu vya magonjwa dhidi ya
dawa katika kongamano la pili la Afya la Sayansi Shirikishi
lililofanyika jijini Dar es Salaam.Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi akitoa maelezo kuhusiana na
kongamano la pili la Afya la Sayansi Shirikishi kuhusu Vimelea Sugu vya
Magonjwa dhidi ya Dawa lililofanyika jijini Dar es Salaam. Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu akizungumza wakati
akifungua kongamano la pili la Afya la Sayansi Shirikishi kuhusu
Vimelea Sugu vya Magonjwa dhidi ya Dawa lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...