Khadija Seif,Michuzi TV
WAZIRI wa
Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye
mahafali ya 15 ya Chuo cha Kodi (ITA) ambayo yatafanyika Novemba
25,2022 chuoni hapo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa habari leo Novemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa
Chuo cha Kodi (ITA) Prof.Isaya Jairo amesema jumla ya wahitimu 489
wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, Stashahada, Shahada na Stashahada ya
Uzamili katika kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.
Amesema ukilinganisha na wahitimu 387 wa mwaka jana 2021, hili ni ongezeko la asilimia 25.1 ya wahitimu wa mwaka huu 2022.
“Ongezeko
hili linatokana na jitihada za Chuo kuhakikisha viwango vya mafunzo
yanayotolewa na Chuo vinakidhi matakwa ya mahitaji ya taaluma na kodi”.
Amesema Prof. Jairo.
Aidha amesema kwa kuzingatia
mahusiano na ushirikiano uliopo kati ya Chuo na Mamlaka za Mapato za
Afrika, Chuo kimewaalika baadhi ya Wakuu wa Mamlaka za Mapato mbalimbali
ambapo tayari baadhi wamethibitisha kushiriki wakiwemo Mamlaka za
Mapato Ghana, Kenya, Eswatini na Malawi.
Amesema
pamoja na Chuo kutoa mafunzo, pia kinatoa ushauri na kuwajengea uwezo
watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bodi ya Mapato Zanzibar
(ZRB) na Mamlaka zingine za Mapato Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...