Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, leo tarehe 12 Novemba, 2022 Dodoma. Kikao hiki ni maandalizi ya kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) kitakacho fanyika siku ya kesho tarehe 13 Novemba, 2022.
Pamoja na mambo mengine vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama walioomba uongozi katika ngazi ya mikoa na Taifa kwa upande wa jumuiya pamoja na chama.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...