-Naibu Waziri Mavunde, Aonesha Imani kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Na; Mwandishi Wetu – Chamwino
Naibu wa Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde, mapema leo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la Membe, litakalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji Wilayani Chamwino, amesema ujenzi unaoendelea wa bwawa hilo unaonesha kuwa, nchi imejiandaa vyema kuhimili na kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi, kutokana na sababu ya bwawa hili kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji ujazo wa lita Bilioni 12 na kuwawezesha wananchi, kufanya shuguli za kilimo, zaidi ya mara moja kwa mwaka na shughuli nyingine za kimaendeleo kama vile za mifugo na uvuvi kwa njia rahisi ambayo pia itaongeza tija katika sekta hizi.
Naibu Waziri Mavunde amesema , bwawa hili ambao litakuwa mkombozi mkubwa sana kwa wakulima katika wilaya ya Chamwino, litakuwa na manufaa ambayo yatapatikana na yatakwenda kubadilisha maisha ya wananchi wa Wilaya hii kiuchumi na kijamiii kutokana na sababu kuwa shughuli hizi zitafanyika kiurahisi kutoka na maji yatakayo patikana katika eneo hili.
Sambamba na hilo Mavunde ameonesha Imani kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupitia kurugenzi wake Mkuu Bw. Raymond Mndolwa, “Nakuamini sana Mkurugenzi Mndolwa na timu yako naamini miradi hii itakuwa kati ya miradi bora, na mradi huu utadumu kwa miaka mingi na kuweza kunufaisha wananchi” Alisema
Aliongeza kusema kuwa “Naamini usimamizi ambao unafanyika hapa ni usimamizi ambao utakwenda sambamba na kuona ubora wa kazi itakayofanyika hapa na iliyokusudiwa.”
Mavunde alionesha matumaini yake ya baadae na kubainisha kuwa kwa baadae eneo hilo litaweza kushawishi utalii wa ndani, hivyo “Naamini wenzetu wa Halmashauri ya Chamwino wataweka miundombinu mizuri ambayo itaweza kushawishi watu kuweza kufika katika eneo hili kwa ajili ya utalii na kufanya shughuli nyingine ambazo pia zitasaidia kuongeza kipato katika Halmashauri yetu, na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja cha kaya na Taifa kwa ujumla.” Alisisitiza
Aliwaasa wananchi Wilaya ya Chamwino hususan kata ya Membe kutoa ushirikiano kwa mkandarasi kwani mradi huo utakwenda kubadilisha wilaya ya Chamwino na kuona matunda ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kulia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavumde akizungumza baada ya ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la Membe litakalotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji lililopo Wilayani Chamwino, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa.
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa Bwawa la Membe Wilayani Chamwino.
Picha ikionesha baadhi ya mafundindi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa Bwawa la Membe Wilayani Chamwino.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...